RAIS Mtarajiwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli (pichani) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Kagame siku ya Jumamosi, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Waziri huyo wa Miundombinu nchini Tanzania, atakuwepo uwanjani wakati wenyeji Yanga SC wakimenyana na Gor Mahia ya Kenya katika mchezo huo wa ufunguzi.
Dk Magufuli amepitishwa na chama chake, CCM mwishoni mwa wiki kugombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Oktoba 25 mwaka huu akiwaangusha vigogo wakiwemo Mawaziri Wakuu wa zamani Frederick Sumaye, Edward Lowassa na Waziri Mkuu wa sasa Mizengo Pinda.
Wakati huo huo kuelekea kuanza kwa michuano ya Kagame siku ya jumamosi, waamuzi wa michezo hiyo wanatarajiwa kuwasili kesho siku ya jumatano sambamba na kamati ya ufundi kwa ajili ya mitihani ya utimamu wa mwili (Physical Test) siku ya alhamisi, na kamati ya ufundi watakua wakikagua viwanja na kuweka vipimo kabla ya ufunguzi rasmi wa michuano hiyo siku ya jumamosi.

0 comments:
Post a Comment