MSHAMBULIAJI Raheem Sterling jana amefunga bao lake la kwanza Manchester City akiichezea kwa mara ya kwanza baada ya kujiunga nayo kutoka Liverpool, ikiibuka na ushindi wa penalti 5-4 baada ya sare ya 2-2 na AS Roma Uwanja wa Kriketi mjini Melbourne.
Katika mchezo huo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu, Sterling alifunga bao lake hilo dakika ya tatu, kabla ya kiungo wa Roma, Miralem Pjanic kusawazisha dakika tatu baadaye.
Kinda wa City, Kelechi Iheanacho akaifungia timu yake bao la pili dakika ya 51 baada ya makosa ya
Ashley Cole aliyetoa pasi ya nyumba kizembe, kabla ya Adem Ljajic kuisawazishia Roma kwa mpira wa adhabu dakika ya 87.
Waliofunga penalti za City ni Yaya Toure, Jesus Navas, Marcos Lopes, Joe Hart na James Horsfield wakati Aleksandar Kolarov alikosa.
Waliofunga penalti za Roma ni Radja Nainggolan, Adem Ljajic, Mattia Destro na Iago Falque wakati
Seydou Doumbia na Seydou Keita walikosa.
Raheem Sterling alitangazwa mchezaji bora mechi baada ya mchezo baada ya kiwango kizuri akiichezea City kwa mara ya kwanza.
Kikosi cha Roma kilikuwa: De Sanctis; Florenzi, Manolas, Romagnoli, Torosidis; Ucan, Pjanic, De Rossi; Iturbe, Totti na Gervinho.
Man City: Caballero/Hart dk46, Sagna/Horsfield dk46, Kompany/Evans dk82, Mangala/Denayer dk46, Clichy/Kolarov dk46, Garcia/Lopes dk46, Fernando/Nasri dk46, Zuculini/Toure dk46, Sterling/Navas dk46, Kelechi/Unal dk73 na Silva/Barker dk46.
Raheem Sterling amefunga bao lake la kwanza Manchester City jana na kuchaguliwa Mchezaji Bora wa Mechi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment