// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NGOMA ‘ALA MWEKUNDU’ MAPEMAAA, YANGA YALAMBWA 2-1 NA GOR MAHIA KAGAME - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NGOMA ‘ALA MWEKUNDU’ MAPEMAAA, YANGA YALAMBWA 2-1 NA GOR MAHIA KAGAME - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, July 18, 2015

    NGOMA ‘ALA MWEKUNDU’ MAPEMAAA, YANGA YALAMBWA 2-1 NA GOR MAHIA KAGAME

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    WENYEJI Yanga SC, leo wameanza vibaya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kufungwa mabao 2-1 na Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Kipigo cha Yanga SC leo kwa kiasi kikubwa kilichangiwa na kucheza pungufu kwa zaidi ya dakika 65, kufuatia mshambuliaji wake, Mzimbabwe Donald Ngoma (pichani kushoto) kutolewa kwa kadi nyekundu mapema kipindi cha kwanza.
    Yanga waliuanza vizuri mchezo huo na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya tano tu kupitia kwa Ngoma aliyepiga mpira mrefu kama krosi kutoka upande wa kushoto na kumbabatiza beki Harun Shakava wa Gor kabla ya kutinga nyavuni.
    Winga Simon Msuva alichangia kuwatibulia hesabu za kuokoa Shakava na kipa wake, Boniface Olouch kutokana na kuifuatilia vizuri krosi ya Ngoma hadi inatinga nyavuni. 
    Bao hilo halikudumu sana, kwani Gor Mahia walifanikiwa kusawazisha dakika ya 18 kupitia kwa na Dirkir Glay aliyepiga shuti kali la mpira wa adhabu lililomshinda kipa Ally Mustafa ‘Barthez’.
    Faulo hiyo ilitolewa baada ya beki wa kulia, Juma Abdul kumuangusha Godfrey Walusimbi nje ya boksi.
    Refa Ssali Mashood alimtoa nje kwa kadi nyekundu Mzimbabwe, Ngoma baada ya kumuonyesha kadi ya pili ya njano kufuatia kumsukuma Shakava wa Gor baada ya kumpamia na mpira hadi nje ya Uwanja dakika ya 25.
    Yanga SC walitulia baada ya kumpoteza Ngoma aliyeondoka uwanjani analia na kuanza kucheza kwa tahadhari kuwanyima nafasi Gor, hali ambayo ilisaidia dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizike timu hizo zikiwa zimefungana 1-1.  
    Kipindi cha pili, Gor Mahia waliingia na mashambulizi ya kulazimisha na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya kwanza tu kupitia kwa mshambuliaji wake, Michael Olunga, aliyewapiga chenga mabeki wa Yanga kabla ya ‘kufyatua’ shuti lililompita Barthez.
    Winga wa Yanga SC, Deus Kaseke (kulia) akimtoka beki wa Gor Mahia, Karim Nzigiyimana
    Donald Ngoma (kulia) akitafuta maarifa ya kumtoka Karim Nzigiyimana
    Kiungo wa Yanga SC, Mbuyu Twite (kulia) akimtoka Meddie Kagere wa Gor Mahia


    Yanga SC walipoteza nafasi nzuri ya kupata sare dakika ya 73, baada ya Nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kumdakisha mkwaju wa penalti kipa Oluoch, kufuatia Shakava kuunawa mpira kwenye boksi.
    Katika mchezo huo uliohudhuriwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Amolo Odinga, kwa ujumla, Yanga SC iliathiriwa na kucheza pungufu.
    Matokeo hayo, yanaifanya Gor Mahia ianzie kileleni mwa Kundi A kwa pointi zake tatu, sawa na KMKM ambayo imeifunga Telecom ya Djibouti 1-0 Uwanja wa Karume leo.
    Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul/Joseph Zuttah dk75, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Simon Msuva/Kpah Sherman dk69, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe, Donald Ngoma na Deus Kaseke/Salum Telela dk84. 
    Gor Mahia; Boniface Olouch, Mussa Mohammed, Sibomana Abouba, Harun Shakava, Kari Nzigiyimana, Dirkir Glay, Khalid Aucho/Erick Ochieng dk89, Godfrey Walusimbi/Ronald Omino dk86, Innocent Wafula/Enock Agwanda dk86, Medie Kagere na Michael Olunga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGOMA ‘ALA MWEKUNDU’ MAPEMAAA, YANGA YALAMBWA 2-1 NA GOR MAHIA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top