Na Princess Asia, DAR ES SALAAM MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amesema kwamba mazoezi ya kujiandaa na msimu katika timu yake mpya, Free State Stars ya Afrika Kusini ni magumu kama ya JKT. Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE kutoka Johannesburg, ambako timu yake imeweka kambi kujiandaa na msimu mpya, Ngassa amesema kwamba anashiriki mazoezi magumu haijawahi kutokea katika kipindi chake chote cha kucheza mpira. “Nina miaka 10 sasa nacheza Ligi Kuu, lakini niseme mwaka huu nimeingia katika timu yenye mazoezi magumu zaidi. Haijawahi kutokea. Mwili wote unauma,”amesema.
Mrisho Khalfan Ngassa (kulia) akiwa hoi baada ya mazoezi ya jana Johannesburg
Ngassa amejiunga na FS ya Bethlehem, Afrika Kusini Mei mwaka huu kama mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wake Yanga SC ya Dar es Salaam. Kiungo huyo mshambuliaji wa zamani wa Toto Africans, Kagera Sugar, Azam FC na Simba SC kwa sasa yuko kambini na timu FS kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini. FS inayofundishwa na Mmalawi, Kinnah Phiri, imeweka kambi yake katika hoteli ya Lake View mjini humo ikijifua asubuhi na jioni kujiandaa na msimu mpya.
Mrisho Ngassa akiwa mazoezini na timu yake jana
Walicheza mechi ya kirafiki mazoezini na Ngassa alianza kikosi cha kwanza
Tayari ratiba ya Ligi Kuu ya ABSA imetoka na FS itafungua dimba na Black Aces kabla ya kukutana na mabingwa watetezi, Kaizer Chiefs katika mchezo wa pili. Kaizer wataanza kutetea taji lao dhidi ya Chippa United Agosti 8. Kwa mujibu wa ratiba ya msimu wa PSL wa 2015-16, Mamelodi Sundowns wataanza na Platinum Stars, Orlando Pirates na SuperSport United, wakati timu mbili zilizopanda msimu huu, Golden Arrows na Jomo Cosmos watakuwa nyumbani na University ya Pretoria na ugenini na Maritzburg United.
Mrisho Ngassa akiteremka kwenye basi jana baada ya kufika Uwanja wa mazoezi
Tayari Ngassa amepata marafiki katika klabu yake hiyo mpya na anaendelea kufurahia maisha ya soka
Afcon Preview: Nigeria host Rwanda
-
Having sealed their Africa Cup of Nations involvement, Nigeria host
Rwanda in Monday’s final qualifying game at Godswill Akpabio Stadium,
aiming to en...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
OMTO WAJA NA MAKUBWA 2024
-
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts
Organization (OMTO), Anna Haule akizungumza wakati mkutano wa kwanza wa
mwak...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment