MFARANSA Morgan Schneiderlin amefungua akaunti yake ya mabao mapema tu Manchester United akiichezea kwa mara ya kwanza kabisa ikishinda 1-0 dhidi ya Club America usiku wa kuamkia leo katika ziara ya kujiandaa na msimu Marekani.
Kiungo huyo alifunga bao hilo pekee katika ushindi huo dakika ya tano tu baada ya kwenda hewani kuifuata krosi ya Juan Mata na kuidondeshea nyavuni.
Morgan Schneiderlin amefungua akaunti yake ya mabao mapema tu Manchester United akiichezea kwa mara ya kwanza kabisa ikishinda 1-0 dhidi ya Club America PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Schneiderlin, Matteo Darmian na Memphis Depay wote walicheza dakika zote 45 mjini Seattle, wakati Bastian Schweinsteiger pia aliichezea kwa mara ya kwanza United baada ya Louis van Gaal kubadilisha wachezaji wote 11 walioanza na kuingiza wengine kipindi cha pili.
Adnan Januzaj na Ander Herrera wote walikaribia kufunga, lakini haikuwa bahati yao na sasa United inaelekea California kucheza na San Jose Earthquakes katika mchezo mwingine kwenye ziara hiyo Jumatano.
Kikosi cha Man United kipindi cha kwanza kilikuwa; Johnstone, Darmian, Jones, Blind, Shaw, Carrick, Schneiderlin, Young, Mata, Memphis na Rooney (Nahodha).
Kipindi cha pili: Lindegaard, McNair, Smalling (Nahodha), Evans, Blackett, Lingard, Schweinsteiger, Herrera, Pereira, Januzaj na Wilson.
Club America: Club America: Gonzalez, Mares/Andrade dk46, Aguilar/Marin dk68, Sambueza (Nahodha), Goltz, Arroyo/Rivera dk68, Samudio/Colula dk68, Guemez/Guerrero dk68, Quintero/Diaz dk68, Martinez/Sanchez dk68 na Buron.
0 comments:
Post a Comment