Memphis Depay akimchambua kipa wa San Jose, David Bingham kuifungia Man United bao la pili katika ushindi wa 3-1 asubuhi ya leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
TIMU ya Manchester United imeshinda mechi ya pili asubuhi hii katika ziara yake ya kujiandaa na msimu nchini Marekani baada ya kuichapa mabao 3-1 San Jose Uwanja wa Avaya mjini San Jose.
Juan Mata alianza kuifungia United dakika ya 32, kabla ya Memphis Depay kufungua akaunti yake ya mabao katika klabu yake mpya kwa bao zuri la pili dakika ya 37.
San Jose wakafanikiwa kupata bao moja dakika ya 42 kupitia kwa Fatai, lakini nyota anayechipukia vizuri Andreas Pereira akafunga bao zuri la kichwa kuihakikishia ushindi timu ya Louis van Gaal.
Kikosi cha Louis van Gaal sasa kitamenyana na mabingwa wa Ulaya, Barcelona katika mchezo ujao wa michuano ya Kombe la Mabingwa wa Kimataifa Jumamosi nchini humo.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa; kipindi cha kwanza; Johnstone, Darmian, Jones, Blind, Shaw, Carrick, Schneiderlin, Young, Mata, Memphis na Rooney.
Kipindi cha pili: Johnstone, McNair, Smalling, Evans, Blackett, Lingard, Schweinsteiger, Herrera, Pereira, Januzaj na Wilson.
San Jose Earthquakes: Bingham, Wynne/Koval dk46, Bernardez/Silva dk62, Goodson/Renato dk46, Stewart/Francis dk46, Alashe, Pierazzi/Pelosi dk46, Garcia/Coutadeur dk46, Cato/Thompson dk46, Salinas/Barrera dk46 na Amarikwa/Sherrod dk46, Jahn dk71.
0 comments:
Post a Comment