// Disable text selection (not fully reliable)
function disableSelection(element) {
element.setAttribute('unselectable', 'on');
element.style.userSelect = 'none';
element.style.MozUserSelect = 'none';
element.style.webkitUserSelect = 'none';
}
// Apply to the entire document body
document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() {
disableSelection(document.body);
});
MECHI YA YANGA NA AZAM FC YANUKIA ROBO FAINALI KAGAME 2015, ITAKUWA JUMATANO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINEMECHI YA YANGA NA AZAM FC YANUKIA ROBO FAINALI KAGAME 2015, ITAKUWA JUMATANO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
MECHI YA YANGA NA AZAM FC YANUKIA ROBO FAINALI KAGAME 2015, ITAKUWA JUMATANO
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM MECHI ya mahasimu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC na Yanga SC inanukia katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki, Kombe la Kagame mapema wiki ijayo. Yanga SC leo wanacheza mechi yao ya mwisho ya Kundi A Kombe la Kagame dhidi ya Khartoum N ya Sudan Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Saa 10:00 jioni. Mchezo huo utatanguliwa na mechi nyingine ya kundi hilo kati ya Gor Mahia ya Kenya na Telecom ya Djibouti. KMKM ya Zanzibar imemaliza mechi zake za kundi hilo na imekwisharejea Zanzibar baada ya kutolewa kufuatia kuambulia pointi tatu za ushindi wa mechi moja dhidi ya vibonde, Telecom 1-0.
Mshambuliaji wa Yanga SC, Kpah Sherman (kushoto) akiwania mpira dhidi ya beki wa Azam FC, Shomary Kapombe katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu. Je, timu hizo zitakutana Robo Fainali Kombe la Kagame? Telecom wamefungwa na kila timu katika kundi hilo na leo wanacheza mechi yao ya mwisho dhidi ya Gor kuanzia Saa 8:00 mchana. Khartoum N na Gor Mahia zote zina pointi saba kila moja baada ya kushinda mechi mbili mbili na kutoa sare moja katika mechi baina yao, wakati Yanga SC ni ya tatu kwa pointi zake sita za ushindi wa mechi mbili. Mshindi wa kwanza wa Kundi A atakutana na Malakia ya Sudan Kusini katika Robo Fainali, mshindi wa pili atakutana na Azam FC wakati mshindi wa tatu atakutana na APR ya Rwanda. Ikiwa sasa inashika nafasi ya tatu, Yanga SC ikifanikiwa kuifunga Khartoum N leo, inaweza ikapanda kileleni iwapo, Telecom watamudu hata kulazimisha sare na Gor Mahia, jambo ambalo halitarajiwi. Matarajio ni Gor kushinda, tena ushindi mnono. Na Yanga SC kuifunga Khartoum N si jambo jepesi pia, kwani timu hiyo inayofundishwa na Mghana Kwesi Appiah imeonyesha ubora wa soka yake katika mechi zilizotangulia. Yanga SC ikiongoza kundi, itacheza na Malakia, ikiwa ya pili itacheza na Azam FC na ikiwa ya tatu itakutana na APR, je itaangukia wapi? Dakika 180 za mechi mbili za leo (Gor Mahia Vs Telecom na Yanga SC Vs Khartoum N) ndiyo zitatoa majibu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam- ila mechi ya Yanga na Azam FC inanukia Robo Kagame 2015.
Mshambuliaji hatari wa Azam FC, Kipre Tchetche jana amefunga mabao mawili katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Adama City
Donald Ngoma amekuwa tishio kwa mabeki wa timu pinzani Kombe la Kagame akiwa na Yanga SC
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
OMTO WAJA NA MAKUBWA 2024
-
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts
Organization (OMTO), Anna Haule akizungumza wakati mkutano wa kwanza wa
mwak...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment