MSHAMBULIAJI Luiz Adriano amemaliza uvumi juu ya mustakabali wake kwa kusaini Mkataba wa miaka mitano na AC Milan.
Mpachika mabao huyo aliyeondoka Shakhtar Donetsk baada ya kuwa na klabu hiyo kwa miaka nane ameigharimu timu hiyo ya Serie A Pauni Milioni 6 kutokana na Mkataba aliokuwa amebakiza.
Mkataba wa Adriano na Shakhtar ulitarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka, lakini Milan imeamua kumsajili sasa kuliko kumsubiri hadi Januari 1 atakapokuwa huru.
Luiz Adriano akiwa na jezi ya AC Milan baada ya kukamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 6 kuhamia kwa vigogo wa Serie A PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Brazil, amefunga mabao 79 katika mechi 162 alizoichezea timu ya Ukraine, yakiwemo tisa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, akiwafuatia Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Neymar ambao wote kila mmoja alifunga mabao 10.
Adriano alikuwa akihusishwa na kuhamia Liverpool wakati fulani, lakini sasa anakwenda kucheza pamoja na Carlos Bacca katika safu mpya ya ushambuliaji ya timu inayotumia Uwanja wa San Siro.
0 comments:
Post a Comment