Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KIPA wa klabu ya AS Vita ya Kongo, Nelson Lukong anatarajiwa kuwasili usiku wa leo Dar es Salaam kuja kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya Azam FC.
Mkongwe huyo atakayefikisha umri wa miaka 35, Oktoba 31, mwaka huu, atawasili na ndege ya Shirika la Kenya.
Lukong alijiunga na AS Vita Club mwaka 2009, akitokea Les Astres ya kwao Cameroon na baada ya kutemwa timu hiyo ya Kongo anakuja kujaribu bahati yake Tanzania.
Tayari Azam FC, imemleta kipa Vincent Atchouailou de Paul Angban kutoka Ivory Coast aliyewahi kudakia timu ya vijana ya Chelsea.
Aidha, kesho asubuhi kiungo Muingereza Ryan Burge atawasili pia kwa ndege ya shirika la Qatar kuja kufanya majaribio, wakati jioni yake kiungo wa Rwanda, Jean Mugiraneze Babtiste atawasili pia kwa ndege ya shirika la Rwanda.
Mugiraneza, au Migi anatokea klabu ya APR ya kwao, wakati Ryan James Burge aliyezaliwa Oktoba 12, mwaka 1988 kwa sasa hana timu tangu alipotemwa na Newport County mwishoni mwa msimu wa 2013/2014.
Wakati anaibuka, kiungo huyo alipewa thamani ya juu na kutabiriwa kuja kuwa miongoni mwa wachezaji wakubwa England. Amewahi pia kufanya majaribio Uholanzi, Japan na England na amechezea Birmingham City, Barnet na Machida Zelvia ya Japan.
Alijiunga na akademi ya Glenn Hoddle nchini Hispania mwaka 2009 kabla ya kupelekwa Worcester City, baadaye Jerez Industrial, Doncaster Rovers na Oxford United kupata uzoefu.
Juni 2011 alisaini Port Vale via Hyde, ambayo ni washirika wa akademi ya Hoddle ambako aliondoka Aprili 2013 baada ya kutofautiana na uongozi na kwenda kusaini Newport County ambako alitemwa mwaka jana.
Azam FC inatarajiwa kuondoka kesho asubuhi kwenda Tanga kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya African Sports Jumamosi na Coastal Union Jumapili Uwanja wa Mkwakwani na itarejea Dar es Salaam Jumatatu kuendelea na maandalizi ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.

Nelson Lukong anakuja kujaribu bahati yake Azam FC |
Ryan Burge anakuja kujaribu bahati yake Azam FC |

0 comments:
Post a Comment