Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KIPA mpya wa Yanga SC, Mudathir Khamis amesema kwamba anawaheshimu makipa wote anaowakuta Yanga SC, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’ kwa sababu wana uzoefu zaidi yake.
Baada ya kusaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na Yanga SC, Mudathir amesema kwamba anatarajia kwenda kuboresha kiwango chake Jangwani.
“Nafurahi nakwenda kufanya kazi na kipa gwiji kabisa Tanzania Juma Pondamali, ambaye ni kocha wa makipa pale Yanga. Lakini pia nakwenda kukutana na makipa wazoefu kuliko mimi Dida na Barhez. Natarajia kwenda kujifunza mengi,”amesema.
Mudathir wiki hii amekamilisha uhamisho wake kutoka KMKM, akisaini Mkataba wa miaka miwili na Yanga SC na anatarajia kuichezea timu hiyo katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, inayoanza kesho Dar es Salaam.
Yanga SC imeweka kambi katika hosteli za Chuo cha Maaskofu, Kurasini, Dar es Salaam ikijifua katika Uwanja wa Chuo cha Polisi jirani na kambini kwao.
Yanga SC wamepangwa Kundi A pamoja na Telecon ya Djibouti, KMKM ya Zanzibar na Gor Mahia ya Kenya ambayo watafungua nayo dimba kesho jioni.
Mechi ya kwanza kabisa ya Kagame 2015 itakuwa ni kati ya KMKM na Telecom Saa 8:00 Uwanja wa Taifa, wakati Saa 10: 00 jioni Yanga watapepetana na Gor Mahia na Uwanja wa Karume APR ya Rwanda itamenyana na Al Shandy ya Sudabn, mchezo wa Kundi B.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Joseph Magufuli ambaye hivi karibuni ameteuliwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Oktoba mwaka huu atakuwa mgeni rasmi katika mechi za ufunguzi Uwanja wa Taifa.

Mudathir Khamis (kulia) akisaini Mkataba wa Yanga SC, huku akishuhudiwa na Katibu Mkuu wa klabu, Dk Jonas Tiboroha |
Mudathir wiki hii amekamilisha uhamisho wake kutoka KMKM, akisaini Mkataba wa miaka miwili na Yanga SC na anatarajia kuichezea timu hiyo katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, inayoanza kesho Dar es Salaam.
Yanga SC imeweka kambi katika hosteli za Chuo cha Maaskofu, Kurasini, Dar es Salaam ikijifua katika Uwanja wa Chuo cha Polisi jirani na kambini kwao.
Yanga SC wamepangwa Kundi A pamoja na Telecon ya Djibouti, KMKM ya Zanzibar na Gor Mahia ya Kenya ambayo watafungua nayo dimba kesho jioni.
Mechi ya kwanza kabisa ya Kagame 2015 itakuwa ni kati ya KMKM na Telecom Saa 8:00 Uwanja wa Taifa, wakati Saa 10: 00 jioni Yanga watapepetana na Gor Mahia na Uwanja wa Karume APR ya Rwanda itamenyana na Al Shandy ya Sudabn, mchezo wa Kundi B.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Joseph Magufuli ambaye hivi karibuni ameteuliwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Oktoba mwaka huu atakuwa mgeni rasmi katika mechi za ufunguzi Uwanja wa Taifa.
0 comments:
Post a Comment