Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KIUNGO chipukizi wa Azam FC, Joseph Kimwaga amesema kwamba anajisikia vizuri kwa sasa na anaamini yuko tayari kwa mechi za ushindani.
Majeruhi huyo wa muda mrefu Azam FC jana alifunga bao moja katika ushindi wa 4-2 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi Friends Rangers Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Na Kimwaga ambaye hajagusa kabisa mpira tangu mwaka jana amesema anajisikia vizuri na anaamini amepona na anaweza kucheza.
“Niko vizuri sana kwa sasa, ninaweza kucheza mechi za ushindani sasa, nina hamu ya kucheza,”amesema.
Hata hivyo, Kimwaga amesema anajua anahitaji kupambana kuonyesha uwezo wake mazoezini ili makocha warejeshe imani kwake na kumrejesha kwenye kikosi cha kwanza.
“Kwa muda ambao nimekuwa sichezi nikijiuguza, wamekuja wachezaji wengine wamechukua nafasi kikosi cha kwanza. Sasa ninaanza upya, natakiwa kupambana kurejesha nafasi yangu,”amesema Kimwaga.
Mchezaji huyo aliyeibukia akademi ya Azam FC, alianza vizuri mwaka juzi alipopandishwa kikosi cha kwanza kabla ya kuumia na kuwa nje kwa kipindi chote hicho.

Joseph Kimwaga kushoto jana alitokea benchi na kwenda kufunga bao moja katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Friends Rangers |
“Niko vizuri sana kwa sasa, ninaweza kucheza mechi za ushindani sasa, nina hamu ya kucheza,”amesema.
Hata hivyo, Kimwaga amesema anajua anahitaji kupambana kuonyesha uwezo wake mazoezini ili makocha warejeshe imani kwake na kumrejesha kwenye kikosi cha kwanza.
“Kwa muda ambao nimekuwa sichezi nikijiuguza, wamekuja wachezaji wengine wamechukua nafasi kikosi cha kwanza. Sasa ninaanza upya, natakiwa kupambana kurejesha nafasi yangu,”amesema Kimwaga.
Mchezaji huyo aliyeibukia akademi ya Azam FC, alianza vizuri mwaka juzi alipopandishwa kikosi cha kwanza kabla ya kuumia na kuwa nje kwa kipindi chote hicho.
0 comments:
Post a Comment