// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIIZA ANAKUJA KUIMALIZA YANGA- HANS POPPE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIIZA ANAKUJA KUIMALIZA YANGA- HANS POPPE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, July 02, 2015

    KIIZA ANAKUJA KUIMALIZA YANGA- HANS POPPE

    Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
    MWENYEKITI Kamati ya Usajili ya Simba Zacharia Hans PopPe amezidi kutupa `Mawe` katika  Nyumba ya Yanga baada ya kuwananga  eti wataendelea kuwanywesha supu ya mawe na kachumbari ya Mwiba hasa baada ya Mshambulizi Hamisi Kiiza kutua Msimbazi.
    Akiongea Ofisini kwake leo `pope` amesema kuwa Ni Kweli kuwa walikaa mezani na Hamisi Kiiza `Diego` na wameshakubaliana  kuitumikia timu hiyo msimu unaotarajiwa kuanza Mwezi ujao.
    ``Kiiza anawasili leo na tumeshamiliza kila kitu ila anakuja kwa masuala ya mwisho ikiwa ni pamoja kumpa mkataba wa miaka miwili na tunaamini ni mchezaji Mzuri  ambaye kwa kushirikiana na wenzake tuliyowasajili tutafanya vizuri``.
    Zacharia Hans Poppe amesema Kiiza anakuja kuwamaliza Yanga 
    Hamisi Kiiza (kushoto) enzi zake Yanga SC akiwa na Abdallah Bin Kleb

    Mwenyeki huyo aliendeleza wimbi lake la kuitupia Yanga  Maneno `magumu` baada ya kusema wataendelea kuchukua  pointi tatu kila wakikutana kwakuwa wao ni bora kuliko Yanga huku akitumia falsafa yake ya supu ya mawe na kachumbari ya miba.
    ``Sisi hatuna shaka hata kidogo kuhusu yanga leongo letu ni kushinda kila mchezo si yanga peke yake lakini hawa watani zetu sisi tutaendelea kuwapa supu ya Mawe na kachumbari ya Miba ni wateja wezu wazuri sana``.
    Mchezaji Hamis Kiiza aliitumikia Yanga kwa misimu miwili   lakini baadaye aliachwa na timu hiyo dakika za mwisho kwa madai ya kushuka kiwango na kudai malipo makubwa ambayo uongozi wa timu hiyo haukuwa tayari kumlipa kwa wakati huo.
    Katika Hatua Nyingine Pope amesema kuwa  wamejifunza mengi kuhusiana na kuajiri makocha na kudai kuwa Kocha aliyekuja kuwatumikia kwa sasa wamempa mkataba usiyozidi mwaka mmoja ili kuwa rahisi kumungozea akifanya vizuri au kupeana mkono wa kwaheri akifanya vibaya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIIZA ANAKUJA KUIMALIZA YANGA- HANS POPPE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top