// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HANS POPE: MESSI NI HAKI YETU TUNAYODHULUMIWA KIMACHOMACHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HANS POPE: MESSI NI HAKI YETU TUNAYODHULUMIWA KIMACHOMACHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, July 10, 2015

    HANS POPE: MESSI NI HAKI YETU TUNAYODHULUMIWA KIMACHOMACHO

    Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
    MWENYEKITI Kamati ya Usajili ya Timu ya Soka ya Simba Zacharia Hans Pope  ni kama ametapika nyongo iliyokuwa ikimsumbua kwa muda mrefu na sasa anahisi mwili wake umeondokana na Nyongo hiyo.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kwa upole na kuonekana ni mtu anayejiamini huku mara kwa mara akionyesha ushahidi wa baadhi ya mikataba yao na Mchezaji Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ pamoja na ushahidi wa maamuzi na maongezi waliyowahi kufanya Pope alikuwa mpole tofauti na alivyozoeleka huku akijiamini.
    Pope aliingia ukumbini mapema akiwasubiri Waandishi wa Habari ambao walianza kuingia saa tano na dakika kumi na Ndipo alipoanza kuongea kuanzia saa tano na dakika 23 mpaka saa saba na dakika 19 alipomaliza huku akionekana kufurahika baada ya kuanika yaliyokuwa moyoni.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe

    Mwenyekiti huyo amesema kuwa suala la Mchezaji Ramadhani Singano lilipangwa na kundi la watu fulani aliyowaita `wenye nia mbaya na simba` ili wauvunje Mkataba wa Mchezaji huyo na kisha akasaini mkataba na Timu ya Azam.
    Amesema kuwa  awali suala lililokuwa likipigiwa kelele ni wao ( Viongozi wa simba) kudaiwa  kuuchezea mkataba wa mchezaji huyo waliyomlea wao wenyewe  jambo ambalo siyo kweli lakini lililoshangaza zaidi ni kubalishiwa tuhuma na kudaiwa kukiuka kifungu kimoja cha mkataba na hivyo mkataba kuvunjwa haraka.
    Ameongeza kuwa mambo yanayoweza kuvunja mkataba ni matatu lakini jambo moja ambalo hata hivyo hawakulikosea limetumika kuuvunja mkataba huo jambo linalokwenda kinyume na kanuni za uvunjwaji wa mikataba.
    ``Hili jambo la sisi kuambiwa tumechezea mkataba wa mchezaji tuliyemlea sisi wenyewe alafu kabla halijaisha wamedaikia jambo jingine linatuumiza kwakuwa sisi tunachafuliwa na tunaonekana kama ni watu wababaishaji ,na tunachotaka sisi ni ukweli ujulikane kuwa sisi siyo wababaishaji tunaobaili maandishi kinyemela`` Alisema Hanspope ambaye leo alionekana kuongea kwakujiamini na kwakituo.
    Amedai kuwa katika moja ya vikao vya usuluhishi mchezaji huyo alikiri kurubuniwa na vilabu vya Yanga na Azam na hivyo alikuwa anatamani mkataba wake umalizike haraka ili aondoke na maamuzi ya kamati hiyo ni dhahiri yalikuwa na shinikizo la timu fulani na kukiuka misingi ya haki.
    `` Upo Ushahidi wakimazingira kuwa azam wamehusika kumrubuni huyo mchezaji  kutokana na mabadiliko tuliyoyaona  ndani ya kamati ,kwakuwa mara ya kwanza tulikubaliana vizuri na sisi mkataba wetu ulikuwa safi hauna kasoro lakini mara yapili tuhuma zikageuzwa na haraka mkataba ukavunjwa bila sisi kupewa nafasi tukalete vielelezo``. Aliongeza Hanspope.
    Ameongeza kuwa baada ya kutokuridhishwa na maamuzi hayo  hayo wataandika barua kwenda shirikisho la soka la nchini TFF kuelezea masikitiko yao na mnamna klabu yao ilivyochafuliwa .
    Katika kamati hiyo Iliyoongozwa na Richard Sinamtwa madai yaliyokuwa yakiikabili Simba ni Uongozi huo kutomlipa Mchezaji huyo kodi ya Pango  huku madai mengine yakiwa ni kutolipa huduma za Afya madai ambayo Uongozi wa Simba ulishinda kwakuthibitisha madai hayo huku suala la kodi ya Pango likijibiwa na Mwenyekiti huyo kamati ya usajili.
    Kwa sakata la Pango Pope amesema, Messi alikuwa akilipwa mshahara wa Sh 700,000 kwa mwezi lakini wao walikuwa wakimpa Sh 800,000, kutokana na laki moja kuwa kodi ya Pango.
    ``Yaani hawa jamaa walikuwa na nia moja tu Kamati ya Sinamtwa imekubali kweli Messi alikuwa akilipwa Sh 800,000 ingawa kwenye mkataba inaonekana ni Sh 700,000 halafu wanasema mkataba unavunjwa kwa sababu hiyo``.. jamani Simba haina haki hapa? Mchezaji tuliyemlea sisi wenyewe?? Aliongeza.
    Katika maswali yanayoulizwa na wadau wa soka ni juu ya utata wa mkataba wa mchezaji huyo wa miaka miwili au mitatu kunyamazishwa ghafla bila kujua aliyekuwa sahihi ni nani? Swali ambalo hata viongozi wa simba wamekuwa wakiuliza bila kupewa majibu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HANS POPE: MESSI NI HAKI YETU TUNAYODHULUMIWA KIMACHOMACHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top