MABINGWA watetezi, Japan wametinga fainali ya Kombe la Dunia wanawake, baada ya kuwafunga England mabao 2-1 usiku wa kuamkia leo.
Japan walipata bao lao la kwanza kwa penalty ya utata, baada ya Claire Rafferty kumuangusha Saori Ariyoshi nje ya boksi, lakini refa akatenga tuta na Aya Miyama akaenda kumtungua Karen Bardsley dakika ya 33.
Dakika saba baadaye, England wakapewa penalti stahili baada ya Steph Houghton Williams kuchezewa rafu na yeye mwenyewe akaenda kufunga bao la kusawazisha dakika ya 40.
Laura Bassett akajifunga dakika ya 90 katika harakati za kuokoa na England wakalala 2-1 na sasa watawania nafasi ya tatu. Laula alilia mno baada ya mchezo huo kiasi cha kubembelezwa na wachezaji wenzake na kocha.
Kikosi cha Japan kilikuwa: Kaihori, Ariyoshi, Iwashimizu, Kumagai, Sameshima, Kawasumi, Utsugi, Sakaguchi, Miyama, Ohno/Iwabuchi dk70 na Ogimi.
England: Bardsley, Bronze/Alex Scott dk75, Houghton, Bassett, Rafferty, Moore, Williams/Carney dk86, Jill Scott, Taylor/White dk60, Chapman na Duggan.
Kocha wa England, Mark Sampson akimbembeleza Laula Bassett baada ya kujifunga dakika ya mwisho dhidi ya Japan PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment