Diamond amelala na tuzo yake jana mjini Durban |
Katika tuzo hiyo, maarufu kama Best Live- Diamond Platnumz amewashinda Big Nuz, Mi Casa wa Afrika Kusini, Flavour wa Nigeria na Toofan wa Togo.
Baada ya ushindi huo; Diamond akasema; “Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa tuzo hii, na pia shukran za dhati ziwafikie wadau, vyombo vya Habari, wasanii na mashabiki wangu wote kwa kunipigia kura na kuhamasisha kwa Nguvu,”.
Diamond pia akaushukuru uongozi wake, familia pamoja na timu nzima ya Wasafi, hususan madansa wake, ambao amesema anaamini ndiyo wamempika akapikika, hadi leo anaweza kuleta tuzo hiyo nzito ya Mtumbuizaji Bora Afrika. “Shukrani za kipekee zimfikie mama yangu kipenzi Sandra kwa mafunzo na malezi anayonipa kila siku juu ya dunia,”aliongeza.
Tanzania iliwakilishwa na wasanii wawili, mwingine ni Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ambaye ‘haikuwa bahati yake’.
Washindi wengine katika tuzo ni, Mwanamuziki Bora wa kike, Yemi Alade wa Nigeria aliwashinda Bucie, Busiswa wa Afrika Kusini, Seyi Shay wa Nigeria na Vanessa Mdee wa Tanzania.
Mwanamuziki Bora wa Kiume, Davido wa Nigeria aliwashinda AKA wa Afrika Kusini, Diamond wa Tanzania, Sarkodie wa Ghana na Wizkid wa Nigeria.
Kundi Bora; P Square wa Nigeria waliwashinda B4 wa Angola, Beatenberg, Black Motion wa Afrika Kusini na Sauti Sol wa Kenya.
Msanii Bora wa Hip Hop; Cassper Nyovest wa Afrika Kusini aliwashinda K.O. wa Afrika Kusini pia, Phyno, Olamide wa Nigeria na Youssoupha wa DRC.
Wimbo bora wa Kushirikiana; All Eyes On Me wa AKA, Burna Boy, Da LES na JR ulizishinda The Sound wa Davido featuring Uhuru na DJ Buckz, Bum Bum wa Diamond na Iyanya, Apero Remix wa Toofan na DJ Arafat na Njama Njama wa Stanley Enow na Sarkodie.
Wimbo Bora wa Mwaka; Dorobucci wa Mavins wa Nigeria ulizishinda Doc Shebeleza wa Cassper Nyovest, Busa wa Euphonik aliyemshirikisha Mpumi, Call Out wa DJ Fisherman na NaakMusiQ waliowashirikisha DJ Tira, Danger na Dream Team, Caracara wa K.O aliyemshirikisha Kid X wote wa Afrika Kusini, Shoki Remix wa Lil Kesh aliyemshirikisha Olamide na Davido, Sura Yako wa Sauti Sol, Gweta wa Toofan, Show You The Money wa Wizkid na Johnny wa Yemi Alade.
Video Bora ya Mwaka ni Nafukwa wa Riky Rick uliozishinda Crazy wa Seyi Shay aliyemshirikisha Wizkid, Doors wa Prime Circle, Love You Everyday wa Bebe Cool, The Sound wa Davido aliyemshirikisha Uhuru na DJ Buckz.
0 comments:
Post a Comment