TIMU ya taifa ya Argentina imetinga fainali ya Copa America 2105 baada ya kuifunga Paraguay mabao 6-1 usiku wa kuamkia leo mjini Concepcion, Chile.
Kwa ushindi huo uliotokana na mabao mawili ya winga wa Manchester United, Angel di Maria na mengine ya Marcos Rojo, Sergio Aguero, Javier Pastore na Gonzalo Higuain, Argentina itakutana na wenyeji Chile katika fainali.
Beki wa Manchester United, Marcos Rojo alianza kuifungia Argentina dakika ya 15, kabla ya Javier Pastore kufunga la pili dakika ya 27 na Lucas Barrios kuwafungia bao la kufutia machozi Paraguay kabla ya mapumziko.
Kipindi cha pili Angel di Maria akaanza ‘balaa lake’ akiifungia Argentina bao la tatu na la nne dakika ya 47 na 53, kabla ya Sergio Aguero kufunga la tano dakika ya 80 na Gonzalo Higuain la sita dakika ya 83.
Kikosi cha Argentina kilikuwa; Romero, Zabaleta, Demichelis, Otamendi, Rojo, Pastore/Banega dk73, Mascherano/Gago dk77, Biglia, Messi, Aguero/Higuain dk81 na Di Maria.
Paraguay; Villar, Valdez/Romero dk56, P Aguilar, Da Silva, Piris, Gonzalez/Bobadilla dk27, V Caceres, Ortiz, Benitez, Haedo na Santa Cruz/Barrios dk30.
Nyota wa Manchester United, Angel Di Maria akishangilia kwa staili yake maarufu ya kukutanisha vidole vyake baada ya kuifungia mabao mawili Argentina katika ushindi wa 6-1 dhidi ya Paraguay PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment