BARAZA la Vyama Vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kesho litaendesha mtihani wa utimamu wa mwili (Pysical test) kwa waamuzi wa watakochezesha michuano ya kombe la Kagame inayoanza mwishoni mwa wiki huu.
Zoezi hilo la utimamu kwa waamuzi watakochezesha mashindano ya Kagame, litafanyika kuanzia saa 2 asubuhi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam litasimamiwa na kamati ya waamuzi yay a CECAFA.
Waamuzi wanaotarajiwa kuhudhuria zoezi hilo ni Ali Ahmed, Suleiman Bashir (Somalia), Ahmed Djama (Djibout), Yetayew Belachew (Ethiopia), Kakunze Herve (Burundi), Davis Omweno, Peter Sabata (Kenya), Issa Kagabo, Hakizimana Louis (Rwanda), Ahemd El Faith (Sudan), Lee Okelo na Mashood Ssali (Uganda), Israel Mjuni na Ferdinand Chacha (Tanzania).
Wakati huo huo: Timu ya Al Shandy kutoka nchini Sudan, Al Malakia kutoka Sudan Kusini na KMKM kutoka Visiwani Zanzibar zinatarajiwa kuwasili kesho jijini Dar es salaam tayari kwa ushiriki wao kwenye michuano ya kombe la Kagame.
Al Shandy wanatarajiwa kuwasili kesho Alhamisi saa 3 kamili asubuhi kwa usafiri wa shirika la Ndega la Kenya (KQ), KMKM wakitarajiwa kuwasili majiraa ya saa 5 kamili asubuhi kwa boti ya Kilimanjaro, na Al Malakia wakitarajiwa kuwasili saa 10 jioni kwa ndege ya Rwanda Air.
Viwanja vya mazoezi vitakavyotumika kwa timu zinazoshiriki michuano ha Kagame ni Chuo cha Ualimu (Duce), TCC – Chang’ombe, Sekondari ya Loyola, Bora Kijitonyama, Polisi Kurasini, Chamazi, Uwanja wa Uhuru.
Timu 11 zitafikia katika hoteli za Durban (Mnazi Mmoja), Chichi (Kinondoni) Ndekha, Grand Villa, Travertine (Magomeni), wakati wenyeji Azam na Yanga watakua na kambi zao kwa ajili ya mashindano hayo.

0 comments:
Post a Comment