MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ubelgiji, Christian Benteke amesema kwamba ametua Liverpool kutoka Aston Villa ili kushinda mataji.
Benteke, aliyejiunga na timu ya Midlands mwaka 2012 na kuifungia mabao 42 katika mechi 88 za ligi, arrived aliwasili viwanja vya mazoezi vya Wekundu hao, Melwood Jumatano baada ya Liverpool kukamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 32.5.
Liverpool pia imewasajili washambuliaji Danny Ings kutoka Burnley, na Roberto Firmino kutoka Hoffenheim, ili kuirejeshea makali safu yao ya ushambuliaji inayomkosa wa muda mrefu, Daniel Sturridge na Luis Suarez aliyehamia Barcelona msimu uliopita na Raheem Sterling aliyetimkia Manchester City.
Christian Benteke amekamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 32.5 kwenda Liverpool kutoka Aston Villa Jumatano PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Akizungumza mara baada ya kukamilisha uhamisho wake, Benteke alisema; "NIna furaha sana kuwa hapa na ningependa kumshukuru mmiliki, Ian (Ayre) na pia kocha kwa jitihada zao za kunifikisha hapa.
"Nafikiri ilikuwa klabu sahihi, kwa sababu nilikuwa nina mawasiliano mazuri na kocha na nilitaka kuwa sehemu ya mipango yake.
"Nafahamu Liverpool ni habari kubwa. Wameshinda mataji mengi ya Ligi Kuu na matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na pia Kombe la UEFA na mataji mengi. Nafahamu ni klabu kubwa.
Alipoulizwa ni kipi kinamhamasisha yeye kama mchezaji, alisema: "Ni juu ya kushinda mataji. Ni kuhusu kufanya kitu fulani katika kazi yangu ambacho naweza labda kuwaeleza wanangu nilichokifanya,".
0 comments:
Post a Comment