// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BANZA STONE ANAZIKWA LEO JIONI MAKABURI YA SINZA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BANZA STONE ANAZIKWA LEO JIONI MAKABURI YA SINZA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, July 18, 2015

    BANZA STONE ANAZIKWA LEO JIONI MAKABURI YA SINZA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
    MWANAMUZIKI Ramadhani Masanja 'Banza Stone' (pichani) anatarajiwa kuzikwa leo jioni makaburi ya Sinza, Dar es Salaam.
    Banza ambaye alizaliwa mwezi wa Ramadhani tarehe 20 mwezi Oktoba, 1972, amefariki katika siku ya mwisho ya kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhani majira ya saa 8 za mchana baada ya kuugua kwa muda. 
    Banza ambaye hapo kabla, alikuwa akizushiwa kifo mara kwa mara, amefariki wakati watu wakitoka ‘mshuko’ wa swala ya Ijumaa. 
    Banza ambaye alizaliwa mwezi wa Ramadhani tarehe 20 mwezi Oktoba, 1972, amefariki katika siku ya mwisho ya kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhani na atazikiwa siku ya Idd Mosi Jumamosi hii Julai 19 kwenye makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam. 
    Msiba wa Banza uko nyumbani kwao Sinza kijiweni jirani kabisa na ulipokuwa msiba wa Steven Kanumba. Mwili wa Banza utalala hapo hapo nyumbani kwao kwa kusubiri taratibu za mazishi siku ya Jumamosi. 
    Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka akizungumza na Waandishi wa Habari jana msibani
    Hali ilivuokuwa msibani jana

    Banza amefia nyumbani kwao ikiwa ni siku chache baada ya kutoka hospitali ya Mwananyamala alikokuwa amelazwa. Banza amefariki kipindi ambacho watu wengi walianza kupata matumaini juu yake kutokana na namna alivyoanza kupata nafuu. Historia ya Banza Stone kimuziki inaanzia kwenye muziki wa disco ambako alikuwa staa kwenye anga hizo akijulikana kama “Banza Mchafu” jina alililoliiba kutoka kwa mpiga bass maarufu wa bendi ya  Maquis. Baadae akapita vikundi kadhaa vya muziki ikiwemo Afri Swezi, Magoma Moto kabla ya kuibukia Twanga Pepeta. Banza akazitumikia TOT, Bambino Sound, Twanga Pepeta kwa mara ya pili, Twanga Chipolopolo, Bambino Sound kwa mara ya pili, Rufita Connection na Extra Bongo. Bendi ya mwisho kwa Banza Stone ni Wana Extra ambayo baadae ilibadilishwa jina na kuwa Rungwe Music Band kabla haijasambaratika mwanzoni mwa mwaka huu. Kwa maana hiyo, Banza Stone ambaye amecha mototo mmoja wa kiume Haji Masanja), amefariki akiwa si mtumishi wa bendi yoyote ile. Miongoni mwa tungo zake zenye mashiko na zinazoheshimika hadi leo hii ni “Kumekucha, “Aunguramapo Simba” na “Mtu Pesa” za Twanga Pepeta wakati TOT alitesa na nyimbo “Mtaji wa Masikini” na “Elimu ya Mjinga”. Wimbo wake wa mwisho kwa upande wa muziki wa dansi ni “Watu na Falsafa” kupitia Extra Bongo mwaka 2013. Banza alikuwa mahiri pia kwa aina nyingine za muziki ikiwemo, mchiriku, taarab na bongo fleva.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BANZA STONE ANAZIKWA LEO JIONI MAKABURI YA SINZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top