Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
AZAM FC imeanza vyema michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kuwafunga KCCA ya Uganda bao 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Shukrani kwake Nahodha, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyefunga bao hilo pekee kipindi cha kwanza na Azam FC sasa inafungana kwa pointi na Malakia ya Sudan Kusini iliyoifunga 2-1 Adama City ya Ethiopia katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo.
Bocco alifunga bao hilo pekee dakika ya 12, kwa guu lake la kushoto akimalizia pasi ya beki wa kulia, Shomari Kapombe.
Bocco angeweza kushangilia bao la pili dakika ya 57 kama asingepiga nje kufuatia krosi nzuri ya Kipre Herman Tchetche aliyetokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Didier Kavumbangu.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Manula Aishi Salum, John Bocco, Pascal Wawa, Agrey Morris, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Didier Kavumbagu/Kipre Tchetche dk46, Morad Said Hussein, Mkami Hamid Mao, Salum Abubakar/Mudathir Yahya dk80 na Frank Domayo/Jean Mugiraneza dk64.
KCCA; Ochan Benjamin, Masiko Tom, Kavuma Habib/Owen Kasuule dk61, Mpuga Martin, Wasswa Hassan, Senkumba Hakim, Okot Denis Oola, Nsibambi Derrick/Shaaban Kondo dk46, Mutyaba Muzamir, Ochaya Joseph na Birungi Michael.

Mfungaji wa bao pekee la Azam FC, John Bocco 'Adebayor' kulia apambana na beki wa KCCA, Joseph Ochaya |
Bocco alifunga bao hilo pekee dakika ya 12, kwa guu lake la kushoto akimalizia pasi ya beki wa kulia, Shomari Kapombe.
Bocco angeweza kushangilia bao la pili dakika ya 57 kama asingepiga nje kufuatia krosi nzuri ya Kipre Herman Tchetche aliyetokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Didier Kavumbangu.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Manula Aishi Salum, John Bocco, Pascal Wawa, Agrey Morris, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Didier Kavumbagu/Kipre Tchetche dk46, Morad Said Hussein, Mkami Hamid Mao, Salum Abubakar/Mudathir Yahya dk80 na Frank Domayo/Jean Mugiraneza dk64.
KCCA; Ochan Benjamin, Masiko Tom, Kavuma Habib/Owen Kasuule dk61, Mpuga Martin, Wasswa Hassan, Senkumba Hakim, Okot Denis Oola, Nsibambi Derrick/Shaaban Kondo dk46, Mutyaba Muzamir, Ochaya Joseph na Birungi Michael.
0 comments:
Post a Comment