Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
AZAM FC wanaingia kambini leo katika hosteli zao za Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam tayari kwa michuano ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Azam FC iliyopangwa Kundi C pamoja na Malakia ya Sudan Kusini, Adama City ya Ethiopia na KCCA ya Uganda, itafungua dimba na KCCA Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Saa 10: 00 jioni.
Mchezo huo utatanguliwa na mechi nyingine kati ya Adama City na Malakia utakaonza Saa 8:00 mchana, wakati jioni Saa 10:00 Uwanja wa Karume, LLB AFC itamenyana na Hegaan FC.
Mechi za utangulizi Jumamosi zitakuwa kati ya
KMKM na Telecom, APR na Shandy na Yanga na Gor Mahia.
APR ipo Kundi B pamoja na Al-Shandy ya Sudan, LLB AFC ya Burundi, Heegan FC ya Somalia na Kundi A kuna wenyeji, Yanga SC, Gor Mahia ya Kenya, Telecom ya Djibout, KMKM ya Zanzibar na Khartoum-N ya Sudan,
Leo Azam FC inatarajiwa kuamua nani akamilishe idadi ya wachezaji wake saba wa kigeni nafasi ambayo kuna uwezekano mkuba ikachukuliwa na mshambuliaji wa Kenya, Alan Wanga.
Katikati ya wiki, Azam FC ilimsajili kiungo wa Rwanda, Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’ aliyeungana na beki Serge Wawa Pascal, kiungo Kipre Michael Balou, mshambuliaji Kipre Tchetche wote kutoka Ivory Coast, winga Brian Majwega kutoka Uganda na mshambuliaji Didier Kavumbangu wa Burundi ambao wote walikuwepo msimu uliopita.
Lakini pia, kuna wachezaji wengine wawili bado wanawania kusajiliwa Azam FC katika nafasi moja iliyobaki, ambao ni kipa Vincent Atchouailou de Paul Angban kutoka Ivory Coast na kiungo Ryan Burge kutoka England.
Awali, Azam FC ilisajili wazalendo tu wawili ambao ni kiungo Ramadhani Singano ‘Messi’ kutoka Simba SC na Ame Ali ‘Zungu’ kutoka Mtibwa Sugar.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall kushoto |

0 comments:
Post a Comment