Kiungo wa APR, Mukunzi Yanick akimtoka kiungo wa Al Shandy, Muhaid Khalid Ahmed mchana wa leo Uwanja wa Taifa |
Katika mchezo huo wa Kundi C, bao pekee la APR lilifungwa na kiungo Bizimana Djihad, dakika ya 64 kwa shuti kali baada ya kupasua katikati ya Uwanja na baada ya kupata upenyo.
Kiungo huyo aliyesajiliwa mapema mwezi huu kutoka kwa mahasimu, Rayon Sport ili kuziba pengo la Jean Baptiste Mugiraneza aliyehamia Azam FC, ni mtoto wa dada wa kiungo wa Yanga SC, Haruna Niyonzima, ambaye pia aliwika Rayon na APR kabla ya kuja Tanzania.
Beki wa Al Shandy, Elsadiq Hassan Musa Ahmed (katikati) akiokoa mpira kwenye eneo la hatari la timu yake, huku kipa wake, Abdelrahman Mukhtar Mohamed akiwa amelala. Kulia ni Mukunzi Yannick wa APR |
0 comments:
Post a Comment