Kiungo Cesaire Gandze alimsababisha Zied Derbali kujifunga kuipatia timu ya Kongo bao la kuongoza kipindi cha kwanza.
KLABU ya AC Leopards ya Kongo imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na CS Sfaxien ya Tunisia 1-1 Uwanja wa Taieb Mhiri jana katika mchezo wa Kundi B Kombe la Shirikisho Afrika.
Matokeo hayo yanamaanisha timu zote mbili hizo mabingwa wa zamani wa Kombe la Shirikisho zimeshindwa kuwasogelea vinara Orlando Pirates na Zamalek, ambao watamenyana leo jioni.
Leopards walianza vizuri mchezo huo na kwa nguvu na kufanikiwa kupata bao ndani ya dakika 20 lakini likakataliwa kwa madai mfungaji alikuwa ameotea.
Mshambuliaji wa CS Sfaxien, Slim Mezlini kisha akakosa mabao mfululizo, huku ‘Juventus ya Uarabuni’ ikisotea ushindi wa nyumbani.
Pamoja na hayo, dakika chache baadaye, Leopards ikapata bao la kuongoza. Kiungo Cesaire Gandze alimsababisha Zied Derbali kujifunga kuipatia timu ya Kongo bao la kuongoza kipindi cha kwanza.
Hata hivyo, bao hilo la Leopards halikudumu, kwani dakika nne tangu kuanza kipindi cha pili, Sfaxien ilifanikiwa kusawazisha wakati Ali Maaloul alipofunga kwa penalti.
Gandze alikaribia kuifungia timu ya Kongo dakika 20 baadaye, lakini akashindwa kufanya hivyo akiwa amebaki yeye na kipa tu Rami Jeridi.
Mechi ijayo, Sfaxien itakuwa mwenyeji wa Orlando Pirates, wakati Leopards watasafiri kuifuata Zamalek wikiendi ya kati ya Julai 24 na 26.

0 comments:
Post a Comment