SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), mwishoni mwa wiki lilifanikisha azma yake ya kukusanya vijana wadogo chini ya umri wa miaka 13 nchi nzima ili kusaka vijana wapatao 60 katika mchakato wa kuunda timu imara ya baaaye ya taifa.
Mashindano ya wiki moja ya vijana chini ya umri wa miaka 13 yaliyoshirikisha karibu mikoa yote ya Tanzania yalifanyika mjini Mwanza na Ilala ikawa bingwa, ikiifunga Alliance Academy ya Mwanza mabao 3-2 katika fainali.
Kwa walioshuhudia michuano hiyo tangu mwanzo, wanasema walijionea dira ya soka ya Tanzania, iwapo kweli TFF itatekeleza programu iliyosema, kuwatunza na kuwalea vizuri vijana hao waje kuwa nyota wa taifa baadaye.
TFF imesema itawalea vijana hao vizuri kwa kuwatengenezea programu tofauti na mafunzo ndani na nje ya nchi, ikiwemo ziara za Ulaya lengo waje kuichezea timu ya vijana ya chini ya umri wa miaka 17 miaka minne ijayo.
Ikumbukwe Tanzania imeomba na kupewa uenyeji wa michuano ya U17 Afrika mwaka 2019 na TFF inataka wakati huo utakapofika iwe na timu imara ya kufika mbali.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema hataki timu hiyo itolewe mapema, anataka ifike mbali, ikibidi ikate tiketi ya kucheza Kombe la Dunia la U17, michuano ambayo timu nne zinazofika Nusu Fainali barani hupata nafasi ya kushiriki.
Ukweli ni kwamba, TFF ya Malinzi imefanya jambo moja zuri sana- kukusanya vijana wadogo na kuanza kutengeneza timu kuanzia chini.
Hata akiondoka madarakani TFF, siku moja Malinzi atakumbukwa kwa mradi huu.
Jambo moja tu, Malinzi anahitaji kuhakikisha anatekeleza ahadi ya kuwaendeleza vijana hao- kwani kwa kufanya hivyo, ndoto zitatimia.
Wakati nikiwapongeza TFF kwa mradi huu na kuwasistiza, wautilie mkazo- umebeba matunda mazuri kwa taifa letu, pia sisiti kuelezea masikitiko yangu juu ya sekta ya mchezo huo kwa ujumla.
Jambo ambalo TFF imefanya hakuna klabu nchini ingeweza kufanya- kukusanya vijana kutoka nchi nzima kutafuta vipaji tofauti vya soka. Hakuna.
Wazi hii ilikuwa ni fursa nzuri kwa klabu zetu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza kutuma wawakilishi wao mjini Mwanza kutafuta vipaji vya kuunda timu zao za vijana.
Unapompata kijana wa umri mdogo chini ya miaka 13 akaanza kuchezea timu yako, wazi huyo akipata maendeleo mazuri na kuwa nyota, basi atakuwa na mapenzi ya dhati na klabu.
Wiki iliyopita nilielezea kuhusu Xavier ‘Xavi’ Hernandez Creus, ambaye Jumamosi ya Juni 6 alicheza mechi yake ya mwisho Barcelona akitokea benchi dakika ya 78 kwenda kuchukua nafasi ya Andres Iniesta katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2015 na kuisaidia Barca kutwaa taji lake la tano la michuano hiyo wakiifunga Juventus ya Italia mabao 3-1 Uwanja wa Olympiki mjini Berlin, Ujerumani.
Hiyo iliifanya Barcelona kuwa klabu ya kwanza kihistoria kushinda mara mbili mataji yote, mawili ya mashindano ya nyumbani na moja la Ulaya, huku Xavi, Iniesta, Lionel Messi, Gerard Pique, Pedro Rodriguez, Sergio Busquets na Dani Alves wakiwa wachezaji pekee waliokuwamo kwenye vikosi vyote vilivyofanya hivyo.
Baada ya mafanikio hayo, Xavi aliyezaliwa Januari 25 mwaka 1980 anahamia Al Sadd ya Qatar kwenda kumalizia soka yake.
Mzaliwa huyo wa mji wa Terrassa, Barcelona, Katalunya, ni zao la akademi ya Barcelona, iitwayo La Masia ambayo alijiunga nayo akiwa ana umri wa miaka 11.
Huyu ni mchezaji ambaye aliibuliwa na Barcelona na alipewa heshima zote wakati anajiandaa kuondoka karibu mwezi mzima sherehe za kumuaga zilifuatana.
Katika wiki hiyo ya Xavi kuagwa, nyumbani Tanzania kulikuwa kuna mgogoro baina ya mchezaji Ramadhani Singano ‘Messi’ na Simba SC, klabu ikidai ilimuibua mchezaji huyo aliyekuwa analalamikia ‘kubambikiwa’ Mkataba kwa mwaka mmoja zaidi.
Messi alitoka Bom Bom kujiunga na Simba SC akiwa tayari mchezaji kijana wa miaka isiyopungua 17- lakini Simba SC kwa kukosa haya, wanasema eti walimuibua!
Leo vigogo wa Ligi Kuu wanashinikiza idadi ya wachezaji wa kigeni iongezwe, kwa sababu wachezaji wa nje wanacheza vizuri na wa nyumbani ‘ili mradi’.
Lakini wanasahau kwamba ipo misingi ambayo imesababisha nchi nyingine kuzalisha wachezaji bora, ambayo kwa hapa kwetu haipo tena.
Mfano mzuri ni kuwa na timu madhubuti za vijana pamoja na programu nzuri za kuwalea na kuwaendeleza. Maulid Dilunga, Sunday Manara, Nico Njohole, Abdallah Kibadeni, Zamoyoni Mogella, Edibily Lunyamila wote ni hawa Watanzania, lakini enzi zao walikuwa wanasoka mahiri na tishio Afrika yote hii, iweje leo tuone Tanzania hakuna wachezaji?
Ni uongo kusema Tanzania hakuna wachezaji. Wachezaji wapo, tatizo hatuna viongozi wa mpira. Kuna watu wajanja wajanja tu, wafanya biashara, watafuta umaarufu na wengine wametumia soka kama ‘kivuli’ cha kukimbilia kukwepa changamoto zao.
Tazama fursa ambayo TFF waliitoa wiki iliyopita, kukusanya mamia ya vijana wadogo nchi nzima- halafu huwezi kuamini hakukuwa na viongozi wa klabu kusaka vipaji.
Lakini ukienda kwenye mifumo yao ya uongozi, haswa hizo klabu kongwe, kuna Kamati za Soka ya Vijana. Lakini hizo Kamati zinaibua wachezaji ambao tayari ‘wamebaleghe’. Tuache kuwasakama wachezaji wa nchi hii, tatizo kuu ni viongozi. Kwaheri, Mungu akipenda Jumapili tena.

0 comments:
Post a Comment