Na Mwandishi Wetu, RADES
TUNISIA imeanza kwa kishindo mechi za Kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuifumua mabao 8-1 Djibouti katika mchezo wa Kundi A jana Uwanja wa Novemba 07 mjini Rades.
Yassine Chikhaoui alifunga mabao matatu peke yake katika ushindi huo, dakika za tisa, 22 na 23, wakati mabao mengine ya Morocco yalifungwa na Ferjani Sassi dakika ya 37, Saber Khalifa dakika ya 68, Fakhreddine Ben Youssef dakika ya 68, Maher Hannachi dakika ya 79 na Yoann Touzghar dakika ya 80.
Bao pekee la Djibouti lilifungwa na Mohamed Liban dakika ya 54. Morocco imeanza na ushindi mwembamba nyumbani wa bao 1-0 dhidi ya Libya mchezo wa Kundi F Uwanja wa Le Grand Stade Agadir, mfungaji Omar El Kaddouri dakika ya 51.
Swaziland wameshinda ugenini mabao 2-1 dhidi ya Guinea mchezo wa Kundi L, mabao yake yote yakifungwa na Tony Tsabedze dakika ya 12 na 84, wakati la wenyeji lilifungwa na Francis Kamano dakika ya 68.
Mechi za kufuzu AFCON ya 2017 zinatarajiwa kuendelea leo na kesho, huku Tanzania ikianzia ugenini dhidi ya Misri kesho.
Leo, Malawi wataikaribisha Zimbabwe Uwanja wa Kamuzu, Afrika Kusini na Gambia Uwanja wa Moses Mabhida, Zambia na Guinea-Bissau Uwanja wa Levy Mwanawasa, Uganda na Botswana Uwanja wa Mandela, Angola na Jamhuri ya Afrika ya Kati Uwanja wa Nacional da Tundavala, Nigeria na Chad Uwanja wa Ahmadu Bello, Cape Verde na Sao Tome Uwanja wa Praia, Burkina Faso na Comoro Uwanja wa Ouagadougou, Mali na Sudan Kusini Uwanja wa Machi 26, Senegal na Burundi Uwanja wa Leopold Sedar Senghor na Algeria na Shelisheli Uwanja wa Mustapha Tchaker.
Kesho, Msumbiji watakuwa wenyeji wa Rwanda Uwanja wa Zimpeto, Ethiopia na Lesotho Uwanjaa wa Addis Ababa, Togo na Liberia Uwanja wa Kegue mjini Lome, Cameroon na Mauritania Uwanja wa Yaounde, Kongo na Kenya Uwanja wa Stade Alphonse Massamba-Debat, DRC na Madagascar Uwanja wa Tata Raphael, Equatorial Guinea na Benin Uwanja wa Bata, Niger na Namibia Uwanja wa Jenerali S.K, Ghana na Mauritius Uwanja wa Ohene Djan, Misri na Tanzania Uwanja wa Borg el Arab, Gabon na Ivory Coast Uwanja wa Libreville na Sudan na Sierra Leone Uwanja wa Khartoum.

![]() |
| Tunisia imeifumua mabao 8-1 Djibouti jana mechi ya kwanza Kundi A kufuzu AFCON ya 2017 |

.png)
0 comments:
Post a Comment