// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TFF YAINGIA MKATABA WA JEZI ZA TAIFA STARS NA GS1 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TFF YAINGIA MKATABA WA JEZI ZA TAIFA STARS NA GS1 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, June 16, 2015

    TFF YAINGIA MKATABA WA JEZI ZA TAIFA STARS NA GS1

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    SHIRIKSHO la Soka Tanzania (TFF) jana limeingia makubaliano na kampuni ya GS1 kwa ajili ya kuweka simbo kwa ajili ya utambuzi wa jezi za timu ya Taifa Stars ili kudhibiti wizi wa jezi za timu hiyo.
    Akizungumza leo mjini Dar es Salaam, Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema kuwa wameamua kuingia makubaliano na kampuni hiyo ili kukabiliana na matatizo  ya uuzwaji wa bidhaa feki ambazo wanakumbana nazo pamoja na wanachama wao.
    Malinzi alisema kuwa baada ya makubaliano hayo sasa 'muarobaini' wa kukomesha tatizo hilo umepatikana.
    Rais wa TFF, Jama Malinzi akionyesha jezi halisi ya Taifa Stars  


    Mkurugenzi wa GS1, Gideon Mazara (kushoto) akimkabidhi Malinzi barcode ya TFF kwa ajili ya jezi za timu za taifa

    "Hii ni hatua ya kwanza ya kusajili Brela, hatua ya pili  kupata alama hii na hatimaye kila mmoja atakayepatikana anauza jezi feki atakamatwa na hatimaye kwenda jela ", alisema Malinzi.
    Naye Mkurugenzi wa kampuni ya GS1 , Gideon Mazara alisema kuwa kampuni yao itaweka alama hiyo na kudhibiti bidhaa za shirikisho hilo.
    Mazara alisema kuwa kwa makubaliano hayo waliyoingia ambapo TFF itatakiwa kulipa ada ya uanachama kila mwaka na hatimaye mapato yatadhibitiwa.
    "Barcode itatatua na suluhisho la matatizo yaliyokuwa yanaisumbua TFF",
    aliongeza Mazara.
    Alisema kuwa kampuni yake inatafanya kazi na makampuni mengine ya hapa nchini 780 ambayo yana bidhaa 13,500 zilizoko sokoni.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAINGIA MKATABA WA JEZI ZA TAIFA STARS NA GS1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top