![]() |
Ramadhani Singano 'Messi' ana matatizo ya Kimkataba na klabu yake, Simba SC |
Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
NI KWELI kuwa Shirikisho la Soka Nchini TFF limetuongezea `utata` katika sakata la Mchezaji Ramadhani Singano badala ya kutupunguzia utata au kutuondolea kabisa.
Kuna mambo ambayo TFF haipaswi kulaumiwa kutokana na kutokuhusika lakini kwahili la Mkataba wa Singano TFF haiwezi kukwepa lawa ya kuongeza utata badala ya kuondoa.
Kwa kila Mchezaji anayesajiliwa anapopewa Mkataba basi na TFF tayari wanamkataba wa Mchezaji huyo na hivyo wanafahamu mwanzo na mwisho wa mkataba.
Ingawa ni kweli kuwa suala la mkataba ni siri ya mwajiri na mwajiriwa lakini kwahili la Mchezaji Singano TFF haikuwa na sababu ya kupata `kigugumizi` kwakuwa lilikuwa limegonga vichwa vya habari na limeleta hisia mbaya juu ya uongozi wa Simba kuwa waliuchezea mkataba huo.
Kwakuwa lilishawachafua Viongozia wa Simba TFF ilipaswa kutoa kauli moja kuwa Uongozi wa Simba haukuhusika `kughushi` mkataba wa Rama.
TFF pia ilipaswa kutoa jimo moja kuwa Ramadhani Singano Ndiye alie `ghushi` Mkataba wake na kutoa hisia hisia zilizopo.
Lakini TFF imekuja na `ukakasi` mkubwa haikutoa jibu moja,imejiuma uma weeeeeh..nakuzidisha utata mkubwa nani afadhali ingekaa kimya kuliko kufanya mamabo ya kitoto hivyo.
TFF kama mnayo mkataba kwanini msiseme mkataba halali ni upi?? Nanyi mna agenda yenu au? Mbona mnawapa waja kusema ile hali walikaa kimya wakisumbuliwa na msongo wa mawazo wa Timu yao ya Taifa!!!!
Inanishangaza kuona TFF inayoujua ukweli inakuja na majibu yenye utata mkubwa eti `waende kuelewana./ waelewane kitu gani? Kwanini Msinyooshe maneno kuwa Mchezaji huyo yu huru? Kwanini msisema bado miaka kumi au mmoja au mitatu?
TFF imeharibu zaidi badala ya kutatua tatizo.
Hivi huyu Mchezaji kwasasa akiafanya mazungumzo na timu Nyingine zaidi ya Simba mtamchukulia hatua? Akishindwa kuelewana na Simba nini kitafuata?
Ninachokiona mimi ni TFF kuzidiwa Nguvu na viongozi wa vilabu ambao wapo ndani ya TFF Jambao ambalo ni upuuzi mtupu .
Hatuna watu wachache kiasi hicho cha kuwafanya viongozi haohao wa vilabu kuwa viongozi Ndani ya TFF .
Kuna Uchafu ndani ya TFF. Sasa kama TFF ilidiriki kumkumbatia `Mhalifu` wa tikiti Bandia itashindwa kumlinda aliyeghushi mkataba ?
Kaeni na uchafu wenu na muendelee kutuzidishia utata katika masuala yanayohitaji uwazi.
(Mwandishi wa makala haya ni Mtangazaji wa Redio One na ITV, ambaye anapatikana kwa namba +255 655 250157 na +255 752 250157)
0 comments:
Post a Comment