WENYEJI Chile wameshinda mabao 5-0 dhidi ya Bolivia katika mchezo wa Kundi A michuano ya Copa America inayoendelea nchini humo.
Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Charles Aranguiz, Alexis Sanchez, Gary Medel pamoja na lingine la kujifunga ambayo yanaipeleka kwenye vita ya kuwania Nusu Fainali timu hiyo.
Aranguiz alifunga mabao mawili, dakika tatu na 66, Sanchez moja dakika ya 37 sawa na Medel dakika ya 79 na Raldes aliyejifunga dakika ya 86 na kwa ushindi huo, Chile inapanda kileleni mwa Kundi A na kutinga Robo Fainali ambako watakutana na mshindi wa tatu bora kutoka makundi yote.
Bolivia imemaliza katika nafasi ya pili na itakutana na mshindi wa pili wa Kundi C.
Kikois cha Chile kilikuwa; Bravo, Isla, Medel, Jara/Pizarro dk70, Beausejour, Diaz, Aranguiz, Valdivia, Vidal/Fernandez dk46, Sanchez/Henriquez dk46 na Vargas.
Bolivia; Quinonez, Rodriquez/M Bejarano dk46, Raldes, Coimbra, Morales, Veizaga, Chumacero, Smedberg, Pedriel, Escobar/Lizio dk61 na Martins.
Katika mchezo uliotangulia, Ecuador imeifunga Mexico mabao 2-1.
Miller Bolanos aliifungia bao la kwanza Ecuador kipindi cha kwanza kabla ya mshambuliaji wa West Ham, Enner Valencia kuongeza la pili kipindi cha pili na Mexico kupata la kufutia machozi kupitia kwa Raul Jimenez, ambalo haliwaepushi kuwa timu ya kwanza kuaga michuano ya Copa America 2015.
Ecuador wamejihakikishia kumaliza nafasi ya tatu na wanaweza kufuzu Robo Fainali kama mshindi wa tatu Bora, itategemea na matokeo ya makundi mengine, B na C katika siku mbili zijazo.
Wachezaji wa Chile wakimpongeza Aranguiz aliyefunga mabao mawili katika ushindi wa 5-0 usiku wa kuamkia leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment