TIMU ya taifa ya Peru imetinga Nusu Fainali ya michuano ya Copa America mwaka 2015 baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bolivia mjini Temuco usiku wa kuamkia leo.
Mshambuliaji wa Corinthians, Paolo Guerrero mwenye umri wa miaka 31 alifunga mabao yote matatu ya Peru katika ushindi huo mnono- la kwanza dakika ya 20 akimalizia krosi, la pili dakika tatu baadaye na la tatu zikiwa zimesalia dakika 16 mchezo kumalizika.
Mshambuliaji wa zamani wa Wigan Athletic, Marcelo Moreno ndiye aliyewafungiaBolovia bao la kufutia machozi kwa penalti dakika ya 84 na sasa Peru watamenyana na wenyeji wa Copa America ya mwaka huu, Chile katika Nusu Fainali mjini Santiago Jumatatu ijayo, Juni 27.
Kikosi cha Peru kilikuwa; Gallese, Advincula, Zambrano, Ascues, Vargas, Retamoso, Yotun, Farfan/Hurtado dk77, Cueva/Reyna dk82, Pizarro/Carillo dk66 na Guerrero.
Bolivia; Quinonez, Hurtado/Escobar dk46, Zenteno, Coimbra, Raldes, Morales/Lizio dk46, Chumacero, Danny Bejarano, Smedberg, Pena/Pedriel dk68 na Martins.
Paolo Guerrero amekuwa shujaa wa Peru kwenye Robo Fainali ya Copa America baada ya kupiga hat-trick wakiitoa Bolivia kwa mabao 3-1 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment