NYANDA za Juu Kusini wametawazwa kuwa mabingwa wa soka kwa wanaume michezo ya Umoja wa Shule za Sekondari wa baada ya kuifunga Dar es Salaam bao 1-0 katika Fainali mjini Mwanza leo.
Nyanda za Juu Kusini walinufaika na bao la kujifunga la wapinzani wao, baada ya mabeki wa Dar es Salaam kujichanganya katika harakati za kuokoa hatari langoni mwao.
Nyanda za Juu Kusini walifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kuifunga Kanda ya Ziwa kwa mabao 3-0, huku Dar es salaam wakitinga hatua hiyo baada ya kuifunga Zanzibar ambao ndio walikuwa mabingwa wa tetezi kwa mabao 4-3.
Katika fainali ya jana wasichana, Dar es salaam wametawazwa kuwa mabingwa baada ya kuwatandika bila huruma Kanda ya Mashariki kwa mabao 7-1, kwenye mchezo uliokuwa na msisimko mkubwa kwa Dar es salaam kuonesha uwezo mkubwa wa kusakata kandanda.
Dar es salaama ilifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kuisukumiza nje Kanda ya Ziwa mabao 4-1,huku Kanda ya Mashariki ikifanikiwa kutinga katika hatua ya fainali baada ya kuifunga Kanda ya Kaskazini kwa mabao 3-1.
Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA chini ya mwenyekiti wake Almas Kasongo, kimeelezwa kufurahishwa kwake na mafanikio yaliyooneshwa na vikosi hivyo vilivyo katika himaya yake (Dar es salaam) na kuviomba vilabu vya ligi mbalimbali kujitokeza kuangalia mashindano ya vijana ili kupata wachezaji wa baadaye kwenye vilabu vyao.

0 comments:
Post a Comment