// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NOOIJ: VIJANA WAKO SAFI KUKATA SHINGO KORONGO LA UGANDA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NOOIJ: VIJANA WAKO SAFI KUKATA SHINGO KORONGO LA UGANDA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, June 19, 2015

    NOOIJ: VIJANA WAKO SAFI KUKATA SHINGO KORONGO LA UGANDA

    KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mart Nooij amesema vijana wake wako katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Uganda.
    Stars, inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kesho inatarajiwa kushuka Uwanja wa Amaan, Zanzibar kumenyana na Korongo wa Uganda katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainaili za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2016.
    Kikosi cha Taifa Stars kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa kuanzia majira ya Saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
    Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij (kulia) amesema vijana wako safi

    Stars inahitaji ushindi katika mchezo huo wa awali ili kujiweka katika mzingira mazuri ya kusonga mbele, kabla ya mchezo wa marudaino utakaofanyika baada ya wiki mbili jijini Kampala.
    Endapo Stars itaitoa Uganda katika hatua ya awali, itafuzu katika hatua ya pili ambapo itacheza dhidi ya timu ya Taifa ya Sudan, na mshindi wa mchezo huo moja kwa moja atafuzu kwa fainali za CHAN 2016 nchini Rwanda.
    Wakati huo huo, timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) inatarajiwa kuwasili leo mchana jijini Dar es salaam kisha kuelekea kisiwani Zanzibar tayari kwa mchezo huo wa kesho dhidi ya Taifa Stars.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NOOIJ: VIJANA WAKO SAFI KUKATA SHINGO KORONGO LA UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top