NAHODHA wa Brazil, Neymar amefungiwa mechi mbili na anaweza kuchukuliwa hatua zaidi za kinidhamu baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu usiku wa kuamkiaa leo, Brazil ikifungwa bao 1-0 na Colombia katika Copa America.
Nyota huyo wa Barcelona alipiga mpira kuelekeza kwa mchezaji wa Colombia, Pablo Armero baada ya mechi kabla ya kutaka 'kumfanyizia' na mfungaji wa bao, Jeison Murillo.
Neymar tayari amepata adhabu ngumu kwa Brazil, kwani ataukosa mchezo wa mwisho wa Kundi C dhidi ya vinara Venezuela Jumapili.
Neymar alitolewa kwa kadi nyekundu dhidi ya Colombia, maana yake atalazimika kuiombea dua Brazil itinge Nusu Fainalo ndipo acheze tena Copa America ya mwaka huu
Pamoja na hayo, refa Enrique Osses hakuwa na namna zaidi ya kumuonyesha Neymar kadi nyekundu ya moja kwa moja, adhabu ambayo pia alimpa mshambuliaji wa Colombia, Carlos Bacca ambaye alianzisha vurugu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, mara moja alikiri kufanya makosa - lakini hakutaka kuomba radhi. "Nilikuwa nina ishu na mmoja wa mabeki wao. Ni kwamba alikuwa ana ishu na mimi, mchezo ulipomalizika na niliposikia kipyenga - nikaupiga mpira na kwenda kumpiga mchezaji wa Colombia. Kisha beki wao akataka kuzinguana na mimi, nikamuangalia tu.
"Nimefanya kosa. Lakini ni sehemu ya mchezo, tumefungwa na tumecheza vibaya. Sikucheza vizuri pia. Nakiri hilo na kuwajibika kwa kilichotokea leo. Sikimbii. Sasa ni juu yetu kushinda mchezo ujao,"amesema mchezaji huyo wa Barcelona.
0 comments:
Post a Comment