KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amefungiwa kuendesha gari kwa miezi sita baada ya kukutwa ya kuendesha kwa kasi mwaka jana.
Mreno huyo alinaswa na kamera akiendesha kwa spidi 60 eneo ambalo alitakiwa kutumia spidi 50 kwa gari lake aina ya A3 Esher bypass mjini Surrey Septemba mwaka 2014.
Katika hukumu iliyotolewa Mahakama ya Staines Magistrates jana, mtu mzima huyo wa umri wa miaka 52 ametakiwa pia kulipa faini ya Pauni 910 kwa kuendesha kwa sspidi 10 zaidi ya kiwango kinachotakiwa.
Jose Mourinho akishereheeka ubingwa wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge baada ya kuiwezesha Chelsea kutwaa taji hilo msimu uliopita
Ametakiwa kulipa Pauni 750 na 75 sambamba na nyingine 85 ya gharama za mahakama.
Mourinho hakutokea mwenyewe mahakamani kusikiliza kesi hiyo. Amezuiwa kuendesha gari kwa sababu tayari ana alama nane katika leseni yake - huku hii ya sasa ikizidi kuchafua rekodi yake.
0 comments:
Post a Comment