Mwandishi Wetu, KAMPALA
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Uganda, The Cranes (Korongo), Milutin ‘Micho’ Sredojevic ameteuwa wachezaji 18 kwa safari ya Zanzibar kuelekea mchezo wa kwanza kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa wa Afrika (CHAN) 2016 utakoafanyika keshokutwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Ni kikosi cha nguvu kabia kutoka nyota wanaocheza Uganda kwa sasa kwa ajili ya mchezo huo wa CHAN, michuano ambayo ni wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee wanaoruhusiwa kushiriki.
“Ni kikosi imara na bora ambacho tuna imani nacho kipo tayari kupambana na kushinda,”amesema Mserbia huyo, Micho akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Kampala leo baada ya kutaja kikosi hicho.
Kikosi hicho ni makipa; Alitho James na Bwete Brian, mabeki; Hassan Wasswa (Nahodha), Denis Okoth, Brian Ochwo, Shafik Bakaki, Deus Bukenya na Derrick Tekkwo
Viungo ni; Yasser Mugerwa, Kizito Keziron, Erisa Sekisambu, Muzamiru Mutyaba, Farouk Miya na Martin Kizza wakati washambuliaji ni; John Semazi, Frank Kalanda, Ssentongo Robert, Fahad na Muhamed Hassan.
Benchi la Ufundi linaongoza na mwenyewe Kocha Mkuu, Micho, Msaidizi wake Moses Basena, Kocha wa Makipa, Fred Kajoba na Daktari Ronald Kisoro.
Wengine ni Mkuu wa Msafara ni Dk. Bernard Patrick Ogwel, Mratibu wa timu Herbert Nsubuga na Ofisa Habari Joseph Mutaka.
Korongo wa Kampala wanatarajiwa kuondoka kesho moja kwa moja hadi Zanzibar na jioni watafanya mazoezi Uwanja wa Amaan kabla ya mechi Jumamosi Saa 2:00 usiku.

0 comments:
Post a Comment