Saturday, June 13, 2015

    MEMPHIS DEPAY NI MCHEZAJI HALALI WA MANCHESTER UNITED

    MSHAMBULIAJI Memphis Depay amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 25 kutua Manchester United akitokea PSV Eindhoven na kuytambulishwa na kocha wake mpya, Louis van Gaal, akimsifia ni mchezaji bora duniani.
    Kinda huyo wa umri wa miaka 21, Depay alivumishwa mno na kuhamia Liverpool, lakini Van Gaal, ambaye alifanya kazi na mpachika mabao huyo alipokuwa kocha wa timu ya gtaifa ya Uholanzi, akawapiku wapinzani wa United, sambamba na mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint-Germain, to Depay katika mbio za kuwania saini yake.
    "Hizi ndoto zilizotimia kwangu; kuchezea klabu kubwa duniani na pia kupata nafasi ya kufanya kazi na mtu mmoja ambaye naamini ni kocha bora duniani, Louis van Gaal,"alisema Depay. "Nina imani kubwa na ninajituma kuhakikisha natimiza ndoto zangu,"aliongeza.
    Memphis Depay akifurahia kutimiza ndoto za kujiunga na United kutoka PSV PICHA ZAIDI NENDA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MEMPHIS DEPAY NI MCHEZAJI HALALI WA MANCHESTER UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry