Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
RAIS wa Shirikisho wa Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema kuwa hatma ya kibarua cha Kocha Mkuu, Mart Nooij kitajulikana ifikapo Julai 4 mwaka huu baadabya mchezo wa marudiano kati ya Taifa Stars na Uganda utakaofąnyika jijini Kampala.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam leo, Malinzi amesema kwamba Kamati ya Utendaji ilifikia maamuzi hayo katika kikao chake kilichofanyika hivi karibuni.
Malinzi alisema kuwa Nooij alipewa mechi tatu na ya kwanza ni dhidi ya Misri ambapo Stars imefungwa mabao 3-0.
Alisema kuwa bado TFF haijabadili msimamo wake dhidi ya kocha huyo raia wa Uholanzi.
Aliongeza kuwa matokeo ya Stars yamewaumiza na hivyo wanataka hali hiyo isiendelee.
"Naomba tukutane Zanzibar Jumamosi katika mechi kati ya Uganda na Tanzania, sina la kusema kwa sasa", aliongeza Malinzi.
Taifa Stars juzi ilifungwa mabao 3-0 na Misri katika mechi yake ya kwanza ya Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 mjini Alexandria.
Mabao yote ya Misri yalipatikana kipindi cha pili, wafungaji Rabia dakika ya 61, Morsi dakika ya 65 na Mohamed Salah dakika ya 70.
Kipigo cha Misri kilikuwa cha nne mfululizo kwa Stars chini ya kocha wake, Mholanzi Mart Nooij baada ya awali kufungwa mechi zote tatu za Kundi B Kombe la COSAFA mwezi uliopita 1-0 na Swaziland, 2-0 na Madagascar na 1-0 na Lesotho mjini Rusternburg Afrika Kusini.
Kwa ujumla huo unakuwa mchezo wa 17 kwa Nooij tangu aanze kuinoa Taifa Stars Aprili mwaka jana akirithi mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen kati ya hizo akiwa ameshinda mechi tatu tu.

Rais wa TFF, Jama Malinzi (kulia) amesema Nooij ataondoka iwapo Taifa Stars itatolewa na Uganda |
Aliongeza kuwa matokeo ya Stars yamewaumiza na hivyo wanataka hali hiyo isiendelee.
"Naomba tukutane Zanzibar Jumamosi katika mechi kati ya Uganda na Tanzania, sina la kusema kwa sasa", aliongeza Malinzi.
Taifa Stars juzi ilifungwa mabao 3-0 na Misri katika mechi yake ya kwanza ya Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 mjini Alexandria.
Mabao yote ya Misri yalipatikana kipindi cha pili, wafungaji Rabia dakika ya 61, Morsi dakika ya 65 na Mohamed Salah dakika ya 70.
Kipigo cha Misri kilikuwa cha nne mfululizo kwa Stars chini ya kocha wake, Mholanzi Mart Nooij baada ya awali kufungwa mechi zote tatu za Kundi B Kombe la COSAFA mwezi uliopita 1-0 na Swaziland, 2-0 na Madagascar na 1-0 na Lesotho mjini Rusternburg Afrika Kusini.
Kwa ujumla huo unakuwa mchezo wa 17 kwa Nooij tangu aanze kuinoa Taifa Stars Aprili mwaka jana akirithi mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen kati ya hizo akiwa ameshinda mechi tatu tu.
0 comments:
Post a Comment