• HABARI MPYA

    Thursday, June 11, 2015

    LEO NI LEO MZEE YUSSUF NA ISHA MASHAUZI NDANI YA VILLA PARK MWANZA

    HATIMAYE ile siku imewadia, tarehe iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa taarab wa jiji la Mwanza ndio hii hapa - ni Mzee Yussuf na Isha Mashauzi katika onyesho la kukata na shoka ndani ya Villa Park leo usiku.
    Ni onyesho linalokutanisha miamba miwili ya taarab ambapo licha ya kuchukuliwa kama mtu na mwanae lakini upinzani mkubwa unatarajiwa kutawala katika onyesho hilo lililopewa jina la usiku wa baba na mwana.
    Wasanii wote wawili (Isha na Mzee) wameahidi kumimina uhondo wa aina yake Alhamisi ya leo hapo Villa Park - Mwanza huku kila mmoja akikataa kuanika silaha (nyimbo) zake za maangamizi.
    Hii ni mara ya kwanza kwa Mzee Yussuf na Isha Mashauzi kukutana jukwaa moja nje ya Dar es Salaam tangu Isha alipojiengua Jahazi Modern Taarab ya Mzee Yussuf zaidi ya miaka minne iliyopita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LEO NI LEO MZEE YUSSUF NA ISHA MASHAUZI NDANI YA VILLA PARK MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top