TIMU ya taifa ya Argentina imewalaza bao 1-0 Uruguay katika mchezo wa Kundi B, michuano ya Copa America usiku wa kuamkia leo mjini La Serena nchini Chile.
Kwa ushindi huo, Argentina inapaa kileleni kwa Kumdi B Copa America 2015, ikiwa na pointi sawa na Paraguay, nne.
Shukrani kwake, mfungaji wa bao hilo pekee Sergio ‘Kun’ Aguero dakika ya 55. Argentina itamaliza na Jamaica mechi ijayo, wakati Uruguay yenye pointi tatu itakutana na Paraguay.
Kocha Gerardo Martino wa Argentina, alipandishwa jukwaani baada ya ‘kuwabwatuia’ marefa.
Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi alicheza, lakini mchezaji mwenzake wa klabu hiyo, Luis Suarez haakuwepo hata benchi.
Kikosi cha Argentina kilikuwa: Romero, Zabaleta, Garay, Otamendi, Rojo, Mascherano, Biglia, Pastore/Banega, Messi, Aguero/Tevez dk82 na Di Maria/Pereyra dk89.
Uruguay: Muslera, M Pereira, Gimenez, Godin, A Pereira, Rios, Rolan, Gonzalez, Lodeiro/Hernandez dk69, C Rodriguez /Sanchez dk64 na Cavani.
Sergio Aguero akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Argentina ikishinda 1-0 dhidi ya Uruguay mjini La Serena PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment