Friday, June 12, 2015

    KIEMBA AZIBA PENGO LA NGASSA STARS, AIFUATA TIMU ADDIS ABABA

    RATIBA YA MECHI ZA KUNDI G

    Jumamosi Juni 13, 2015
    Nigeria v Chad
    Misri v Tanzania
    Jumamosi Sept 5, 2015
    Tanzania v Nigeria
    Chad v Misri
    Ijumaa Machi 25, 2016
    Chad v Tanzania
    Nigeria v Misri
    Jumatatu Machi 28, 2016
    Tanzania v Chad
    Misri v Nigeria
    Jumamosi Juni 4, 2016
    Chad v Nigeria
    Tanzania v Misri
    Jumamosi Sept 3, 2016
    Nigeria v Tanzania
    Misri v Chad
    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KIUNGO Amri Ramadhani Kiemba ameondoka leo Dar es Salaam kwenda Addis Ababa, Ethiopia kuungana na timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa safari ya Misri.
    Taifa Stars inakwenda Misri baadaye leo kwa ajili a mchezo wa kwanza wa Kundi G kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 nchini Gabon dhidi ya Misri. 
    Kiemba alikuwa katika kikosi cha pili cha timu ya taifa, chini ya kocha Salum Mayanga ambacho kilikwenda Rwanda kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji, wakati Taifa Stars A inakwenda kambini Ethiopia.
    Na kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij amelazimika kumuita Kiemba baada ya kumkosa kiungo mshambuliaji, Mrisho Khalfan Ngassa ambaye ametingwa na shughuli binafsi.  
    Kwa mujibu wa Mkuu wa Msafara wa Taifa Stars, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ maandalizi ya timu ni mazuri na kuna matumaini makubwa ya ushindi wa ugenini.
    “Kwa kweli maandalizi yetu hapa Addis yamekuwa mazuri sana, vijana wamefanya mazoezi katika mazingira mazuri na wapo vizuri kabisa. Ni kwamba tuna matumaini makubwa ya ushindi wa ugenini,”amesema Kaburu.
    Amri Kiemba akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam leo kwa safari ya Addis Ababa
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIEMBA AZIBA PENGO LA NGASSA STARS, AIFUATA TIMU ADDIS ABABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry