// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CHUJI, SHILOLE WAITWA TIMU YA TAIFA YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 15 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CHUJI, SHILOLE WAITWA TIMU YA TAIFA YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 15 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, June 18, 2015

    CHUJI, SHILOLE WAITWA TIMU YA TAIFA YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 15

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    MFUNGAJI bora wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 13 iliyomalizika mwishoni wiki mjini Mwanza, Morris Michael Njaku ‘Chuji’ (pichani juu) ameorodheshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana umri chini ya miaka 15.
    U-15 itaingia kambini Jumatatu ya Juni 22 kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya kombaini ya mkoa wa Mbeya, utakaofanyika mjini Mbeya Juni 28, mwaka huu.
    Kikosi hicho kinaandaliwa kwa ajili ya mechi za mtoano kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitakazofanyia nchini Madagascar mwaka 2017. Hatua ya mtoano wa awali itaanza mwakani 2016 mwezi Juni.
    Timu itakua chini ya kocha Bakari Shime kwa muda akisaidiwa na Peter Manyika. Kocha aliyekua ameteuliwa awali kufundisha timu hiyo Adolf Rishard ameomba udhuru baada ya kupata fursa ya kwenda masomoni.
    Wachezaji watakaoingia kambini na mikoa wanayotokea kwenye mabano ni Mwinjuma Yahya (Tanga), David Mpakazi, Shilole Anthony (Geita), Kibwana Shomari , Ibrahim Koba, (Morogoro), Faraji John, Kelvin Deogratius, Davison Meddy, Maulid Lembe (Dodoma), Ally Msengi (Mwanza).
    Wengine ni Timoth Timothy, Juma Juma, Pius Raphael, Mohamed Ally (Dodoma), Athumani Rajabu, Juma Zubeir, Jonathan Rafael (Kigoma), Robert Philip, Jaffari Juma (Arusha), Michael Kanuti, Alex Peter, Rashid Kilongola (Kinondoni), Morris Michael (Ilala), Karim Mfaume (Lindi), Assad Juma (Unguja Magharibi), Francis Mrope, Kelvin Pius (Mara).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHUJI, SHILOLE WAITWA TIMU YA TAIFA YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 15 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top