WENYEJI Chile wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 3-3 na Mexico usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Kundi A michuano ya Copa America.
Matokeo hayo yanaipandisha kileleni Chile Kundi A kwa wastani wa mabao baada ya kufungana pointi na Bolivia.
Mabao ya Mexico yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Manchester City, Vicente Vuoso mawili dakika za 21 na 66, lingine Jimenez dakika ya 29, wakati ya Chile yalifungwa na Arturo Vidal mawili dakika za 23 na 55 kwa penalti lingine Vargas dakika ya 42.
Chile itacheza na Bolivia katika mchezo wa mwisho wa kundi lao wakati Mexico itamaliza na Ecuador.
Kikosi cha Chile kilikuwa; Bravo, Albornoz/Beausejour dk87, Medel, Jara, Isla, Diaz/Mena dk71, Aranguiz, Vidal, Valdivia, Sanchez na Vargas/Pinilla dk85.
Mexico; J Corona, Ayala, Dominguez, Valenzuela, Flores, Alderete/Salcedo dk71, Guemez, JM Corona/Osuna dk77, Medina/Aquino dk64, Vuoso na Jimenez.
Arturo Vidal akijaribu kuuinua umati wa mashabiki baada ya kufunga bao katika sare ya 3-3 na Mexico PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment