WENYEJI Chile wamefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Copa America kwa ushindi wa bao 1-0 Uwanja wa Nacional Julio Martinez Pradanos mjini Santiago dhidi ya Uruguay.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Sandro Meira Ricci wa Brazil, Uruguay ilipoteza wachezaji wawili waliotolewa kwa kadi nyekunfu, Edinson Cavani kwa kumtolea ‘maneno ya shombo’ refa na kumzaba kibao Gonzalo Jara aliyemtia 'dole' nyuma- na Jorge Fucile aliyemchezea rafu Alexis Sanchez.
Shujaa wa Chile usiku wa kuamkia leo alikuwa Mauricio Isla aliyefunga bao hilo zikiwa zimesalia dakika 10 mchezo kumalizika mjini Santiago.
Katika Nusu Fainali wiki ijayo, Chile sasa watakutana na mshindi kati ya Bolivia dhidi ya Peru, wanaomenyana leo katika Robo Fainali.
Kikosi cha Chile kilikuwa; Bravo, Isla, Medel, Jara, Mena, Aranguiz, Diaz/Fernandez dk71, Vidal, Valdivia/Pizarro dk85, Sanchez na Vargas/Pinilla dk71.
Uruguay; Muslera, Pereira, Gimenez, Godin, Fucile, Sanchez/J Rodriguez dk85, Rios, Gonzalez, C Rodriguez, Rolan/Hernandez dk58 na Cavani.
Arturo Vidal akiwarukia wachezaji wenzake wa Chile kuungana na nao kumpongeza mfungaji wa bao lao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Uruguay, Mauricio Isla usiku wa Jumatano PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment