TIMU ya taifa ya Brazil imechapwa bao 1-0 na Colombia usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Kundi C michuano ya Copa America inayoendelea Chile.
Wachezaji Neymar na Carlos Bacca walionyeshwa kadi nyekundu mwishoni mwa mchezo baada ya kugombana.
Bao pekee la Colombia lilifungwa na Jeison Murillo dakika ya 36, wakati kwa mara nyingine mshambuliaji Radamel Falcao alichemsha na kutolewa.
Matokeo hayo yanaifanya Colombia ijiokotee pointi tatu za kwanza na kuwa sawa na Brazil na Venezuela inayojutuliza kileleni mwa Kundi C kwa wastani wa mabao.
Timu hizo zilikutana katika Robo Fainali ya Kombe la Dunia mwaka jana na Brazil ikashinda 2-1.
Kikosi cha Brazil kilikuwa: Jefferson, Alves, Silva, Miranda, Filipe Luis, Fernandinho, Elias/Tardelli dk76, Willian/Costa dk69, Neymar, Fred/Coutinho dk46 na Firmino.
Colombia: Ospina, Zuniga, Zapata, Murillo, Armero, Sanchez, Valencia/Mejia dk80, Cuadrado, James, Gutierrez/Bacca dk76 na Falcao/Ibarbo dk69.
Neymar akidhibitiwa na beki wa Colombia, Carlos Sanchez katika mchezo huo jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment