Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
AZAM FC ipo katika harakati za kumsajili beki hodari wa kati wa kimataifa wa Rwanda, Jean-Baptiste Mugiraneza ‘Migi’ (pichani kulia).
BIN ZUBEIRY inafahamu mazungumzo baina ya klabu na mchezaji huyo aliyezaliwa Februari 17, mwaka 1992 mjini Kigali yamekwishafanyika na makubaliano yamefikiwa.
Beki huyo wa APR FC ya Rwanda amekubali kujiunga na Azam FC baada ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame ambayo itafanyika mwezi ujao Dar es Salaam.
Na Azam FC inategemea majibu ya Azimio la Zanzibar, kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) visiwani humo kesho kuamua juu ya idadi ya wachezaji wa kigeni.
Kwa sasa kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaruhusu wachezaji watano tu wa kigeni, lakini baada ya shinikizo la vigogo, mchakato wa kuongeza idadi umefikia ‘patamu’.
Kurugenzi ya Ufundi iliagizwa na Kamati ya Utendaji mwezi uliopita kupitia mapendekezo ya klabu juu ya idadi ya wachezaji wa kigeni na kuyawasilisha kwa Kamati ya Mashindano ambayo pia ilipaswa kuyapitia na kutoa maoni yake- ambayo sasa yanapelekwa Kamati ya Utendaji tena kutolewa majibu.
Ingawa mapendekezo ya klabu ni wachezaji 10, lakini Kurugenzi ya Ufundi ilipendekeza wawe saba na Kamati ya Mashindano inataka wawe wanane.
Iwapo idadi yoyote itaongezwa kutoka watano, wazi Migi aliyeibukia SC Kiyovu Sport kabla ya kusaini APR FC mwaka 2007 atakuwa na nafasi ya kuwa miongoni mwa wachezaji wapya wa kigeni wa Azam FC.
Wakati fulani, Migi alivumishwa sana kuhamia Stade Rennais F.C. ya Ufaransa- na Februari 9 mwaka 2009 vyombo vya habari Rwanda viliandika kwa uzito mkubwa Migi kutakiwa na Rennais, ingawa mpango huo ‘ulikufa’ kimya kimya.
Hadi sasa, Azam FC imesajili mchezaji mmoja tu mpya, mzalendo Ame Ally ‘Zungu’ kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro- wakati tayari imefikia makubaliano na kipa wa kimataifa wa Ivory Coast, aliyewahi kudakia timu ya vijana na ya wachezaji wa akiba ya Chelsea FC ya England, Vincent Atchouailou de Paul Angban.
Angban ambaye kwa sasa anadakia klabu ya Jeunesse ya Ligi Kuu ya kwao, Ivory Coast, anatarajiwa kuwasili wiki ijayo kwa ajili ya kusaini Mkataba wa kujiunga na Azam FC.

0 comments:
Post a Comment