// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC KUMKOSA MCHA KOMBE LA KAGAME, AFUNGWA 'POP' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC KUMKOSA MCHA KOMBE LA KAGAME, AFUNGWA 'POP' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, June 18, 2015

    AZAM FC KUMKOSA MCHA KOMBE LA KAGAME, AFUNGWA 'POP'

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Mcha Khamis 'Vialli' (pichani) ataikosa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame kufuatia kufungwa plasta gumu (PoP) kwenye mguu wake wa kushoto kutokana na maumivu ya goti la mguu wa kushoto.
    Kwa mujibu wa daktari wa Azam, Mbaruku Mlinga, Mcha atakuwa nje kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa na Kombe la Kagame linatarajiwa kuanza wiki ya pili ya mwezi ujao.
    "Alivunjika kidogo kwenye goti ndiyo maana tukamwekea PoP ili awe sawa. Atakaa na PoP hilo kwa muda wa wiki mbili na tangu alipowekwa hadi leo, ameshamaliza wiki moja hivyo Alhamisi ijayo atatolewa,"alisema Mbarouk.
    "Baada ya hapo, ataanza mazoezi mepesi kama wiki mbili ndiyo atarudi uwanjani akiwa vizuri kabisa na kwa maana hiyo, upo uwezekano akakosa mashindano ya Kagame."
    Mbaruku amesema, wachezaji wengine ambao wana program maalum ni beki wa kushoto, Waziri Salum aliumia unyayo Congo, beki wa kati, Abdalah Kheri alichanika nyama paja na program anayofanya ni kuweka sawa, jeraha lisiweke kovu.
    Wengine ni Joseph Kimwaga aliyefanyiwa upasuaji Afrika Kusini na programu yake ni kumfanya apone kabisa na Farid Mussa alikuwa anasumbuliwa na nyama za paja amepona kabisa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC KUMKOSA MCHA KOMBE LA KAGAME, AFUNGWA 'POP' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top