KLABU ya Arsenal imekamilisha usajili ya kipa wa Chelsea, Petr Cech na mlinda mlango huyo anaweza kukutana mapema na klabu yake ya zamani, kwani timu hizo mbili zitamenyana Agosti 2 katika mechi ya Ngao ya Jamii Uwanja wa Wembley.
Mazungumzo juu ya dili hilo la Pauni Milioni 11 yamekuwa yakiendelea tangu kumalizika kwa msimu ulkiopita na kocha wa Arsenal, Arsene Wenger hatimaye amemnasa kipa huyo mwenye umri wa miaka 33.
Jose Mourinho alikuwa anasita kumuuza Cech kwa wapinzani wake hao katika Ligi Kuu ya England, na pamoja na taarifa za kukamilika kwa dili hilo, bado hakuna taarifa rasmi zilizotolewa.
Petr Cech amekamilosha uhamisho wake kutoka Chelsea kwenda Arsenal kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya England
Paris Saint-Germain inafahamika iliwasilisa maombi rasmi Chelsea kutaka kumnunua kipa huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech, ambaye ameamua kubaki London ambako familia yake ipo.
Cech alitaka mwenyewe kuondoka Chelsea baada ya kupokonywa namba na Mbelgiji Thibaut Courtois katika kikosi cha kwanza cha The Bluse katika msimu ambao timu hiyo ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich amemfungulia milango ya kutokea.
Kuwasili kwa Cech The Gunners kunamaanisha mmoja wao kati ya Wojciech Szczesny au David Ospina, ambaye anatakiwa na Fenerbahce, anaweza kuondoka kabla ya msimu mpya.
0 comments:
Post a Comment