AC Milan leo imemfukuza kocha Filippo Inzaghi baada ya msimu mbaya na mara moja imemchukua Mserbia, Sinisa Mihajlovic.
Milan haitashiriki michuano ya Ulaya msimu ujao, baada ya kumaliza nafasi za chini katika msimamo wa Serie A sambamba na mahasimu wao wa jiji, Inter ambayo ndiyo imesababaisha mwisho wa Inzaghi.
Mkali huyo wa mabao wa zamani Ulaya, alishindwa kufufua makali ya Milan baada ya kurithi mikoba ya mchezaji mwenzake wa zamani wa timu hiyo, Clarence Seedorf msimu uliopita.
"AC Milan inatangaza kwamba imemfukuza kocha Filippo Inzaghi, ambaye inamshukuru kwa kazi aliyoifanya," taarifa ya klabu hiyo ya Serie A imesema.
Kocha wa zamani wa Sampdoria, Mihajlovic amesaini Mkataba wa miaka miwili na Milan, mabingwa mara saba wa Ulaya.
Inzaghi, ambaye alipewa jina la utani Superpippo, alijipatia umaarufu akiwa mchezaji Milan, akifunga mabao 126 katika mechi 300 na kushinda mataji 10 yakiwemo mawili ya Ligi ya Mabingwa.
Lakini mkongwe huyo wa umri wa miaka 41 heshima yake imeshuka taratibu tangu arithi mikoba ya Seedorf Juni Juni mwaka 2014.
Bilionea mmiliki wa Milan, Silvio Berlusconi amekiri kuwa na dora tofuati na Inzaghi katika klabu hiyo. Milan ilimaliza katika nafasi ya 10 katika msimu huu wa Serie A, ambayo ni nafasi mbaya zaidi tangu Berlusconi aichukue klabu hiyo miongo mitatu iliyopita.

0 comments:
Post a Comment