![]() |
Mchezaji wa Zambia akienda chini baada yaa kukwatuliwa na beki wa Ghana |
Zambia imewafunga Ghana mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza jana kabla ya Malawi kuwang’oa wenyeji, Afrika Kusini kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 0-0.
Mabao ya waliokuwa mabingwa watetezi wa COSAFA, Zambia yalifungwa na Bornwell Mwape, Aaron Katebe na Nathan Sinkala.
Ghana watakutana na Bafana Bafana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.
Michuano ya wababe ya COSAFA leo inaingia katika hatua ya Nusu Fainali, Namibia ikimenyana na Madagascar Uwanja wa Moruleng Saa 11:00 jioni na baadaye Saa 1:00 usiku Botswana watamenyana na Msumbiji.
Wachezaji wa Malawi (kulia) na Afrika Kusini (kushoto) wakigombea mpira jana
0 comments:
Post a Comment