// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC WAUJARIBU UWANJA WA OLIMPIKI AMBAO KESHO WATAMENYANA NA ETOILE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC WAUJARIBU UWANJA WA OLIMPIKI AMBAO KESHO WATAMENYANA NA ETOILE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, May 01, 2015

    YANGA SC WAUJARIBU UWANJA WA OLIMPIKI AMBAO KESHO WATAMENYANA NA ETOILE

    Na Prince Akbar, TUNIS
    YANGA SC leo wanatarajiwa kufanya mazoezi katika Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse, Tunisia ambao kesho utatumika kwa mchezo dhidi ya wenyeji wao, Etoile du Sahel kuanzia Saa 1:00 usiku kwa saa za Kaskazini mwa Afrika na Saa 3:00 kwa saa za Afrika Mashariki.
    Yanga SC watakuwa wageni wa Etoile kwenye Uwanja huo wenye kuchukua mashabiki 28,000 tu katika mchezo wa marudiano, hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika.
    Yanga SC wanatakiwa kulazimisha ushindi wa ugenini, au sare ya kuanzia mabao 2-2 ili kusonga mbele, baada ya awali kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani, Dar e Salaam.
    Wachezaji wa Yanga SC katika hoteli waliyofikia mjini Sousse
    Andrey Coutinho kulia na Salum Telela kushoto wakipata mlowa asubuhi ya leo hotelini hapo
    Nizar Khalfan akipata mlo wa asubuhi
    Basi wanalotumia Yanga SC nchini Tunisia

    Sare nyingine ya 1-1 itaurefusha mchezo huo hadi kwenye dakika 120 na ikishindikana pia kupatikana mshindi, penalti zitachukua nafasi ya kutoa hukumu ya timu ya kusonga mbele.
    Yanga SC iliwasili jana jioni mjini Tunis na baada ya kugandishwa kwa saa zaidi ya mbili Uwanja wa Tunis, ikasafiri kwa basi kuelekea mji mdogo wa Sousse kwa wenyeji wao, Etoile du Sahel umbali wa kilomita 140.
    Yanga SC imefikia katika hoteli nzuri, El Mouradi Palm Marina na jana baada ya kuwasili tu Sousse ilikwenda kufanya mazoezi katika Uwanja wa jirani, mwendo wa dakika 20 kwa gari.
    Yanga SC iliondoka Dar es Salaam usiku wa juzi na kwa bahati mbaya, kiungo wake tegemeo mchezeshaji, Haruna Niyonzima amebaki kutokana na kuwa majeruhi.
    Wachezaji walio na Yanga SC Tunisia ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’, mabeki Pato Ngonyani, Oscar Joshua, Edward Charles, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ’Juma Abdul, Rajab Zahir, Mbuyu Twite na Kevin Yondan.
    Viungo ni Nizar Khalfan, Andrey Coutinho, Salum Telela na Said Juma ‘Makapu’, wakati washambuliaji ni Hussein Javu, Amissi Tambwe, Kpah Sherman, Mrisho Ngasa, Jerry Tegete na Simon Msuva. 
    Iwapo Yanga SC itafanikiwa kuitoa Etoile, itaingia katika kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho, ikicheza na moja ya timu zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Mwaka jana, Yanga SC ilicheza Ligi ya Mabingwa Afrika na kutolewa katika hatua ya 32 Bora na Al Ahly ya Misri kwa penalti, 4-3 baada ya sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani kwake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WAUJARIBU UWANJA WA OLIMPIKI AMBAO KESHO WATAMENYANA NA ETOILE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top