Na Prince Akbar, SOUSSE
YANGA SC wamefanya mazoezi katika Uwanja wa mpira wa kikapu asubuhi ya leo kuelekea mchezo wa usiku wa leo dhidi ya wenyeji Etoile du Sahel.
Uwanja huo upo katika hoteli waliyofikia, El Mouradi Palm Marina na kocha Hans van der Pluijm aliamua vijana wake wafanye mazoezi kidogo hapo ili kuiweka miili sawa kabla ya mchezo huo,
Yanga watakuwa wageni wa Etoile du Sahel Uwanja wa Olimpiki, Sousse katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga SC waliofika juzi usiku Tunisia, wanahitaji ushindi wa ugenini au sare ya zaidi ya mabao 2-2 ili kusonga mbele, baada ya awali kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani Dar es Salaam.
Sare nyingine ya 1-1 itaurefusha mchezo huo hadi kwenye dakika 120 ambako pia mshindi asipopatikana mikwaju ya penalti itatumika.
Refa Mganda, Dennis Batte aliyefupisha safari ya Tanzania katika mbio za Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2015 Equatorial Guinea, ndiye atachezesha mchezo huo leo.
Batte atasaidiwa na Waganda wenzake, Mark Ssonko na Balikoowa Musa Ngobi, ambao watakuwa washika vibendera. Mwamuzi wa akiba pia atatoka huko, wakati Kamisaa atatoka nchi nyingine.
Batte ‘aliiuma’ Taifa Stars wazi wazi ikifungwa mabao 2-1 na wenyeji Msumbiji Agosti 3, mwaka jana Uwanja wa Zimpeto mjini Maputo katika mchezo wa marudiano, hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza fainali hizo ambazo awali ilikuwa zipigwe Morocco.
Televisheni namba moja Tanzania ya michezo na burudani- Azam TV itaonyesha moja kwa moja mechi hiyo kutoka Tunisia kuanzia Saa 1:00 usiku kwa Saa za Kaskazini mwa Afrika na Saa 3:00 usiku kwa Saa za Afrika Mashariki.
Etoile du Sahel wamethibitisha kufikia makubaliano na Azam TV kurusha mchezo huo ‘Live’ leo.

Wachezaji wa Yanga SC wakifanya mazoezi Uwanja wa mpira wa kikapu leo asubuhi |
Uwanja huo upo katika hoteli waliyofikia mjini Sousse |
Baada ya mazoezi wakapata mlo wa mchana na kwenda kupumzika kusubiri muda wa kwenda uwanjani |
Sare nyingine ya 1-1 itaurefusha mchezo huo hadi kwenye dakika 120 ambako pia mshindi asipopatikana mikwaju ya penalti itatumika.
Refa Mganda, Dennis Batte aliyefupisha safari ya Tanzania katika mbio za Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2015 Equatorial Guinea, ndiye atachezesha mchezo huo leo.
Batte atasaidiwa na Waganda wenzake, Mark Ssonko na Balikoowa Musa Ngobi, ambao watakuwa washika vibendera. Mwamuzi wa akiba pia atatoka huko, wakati Kamisaa atatoka nchi nyingine.
Batte ‘aliiuma’ Taifa Stars wazi wazi ikifungwa mabao 2-1 na wenyeji Msumbiji Agosti 3, mwaka jana Uwanja wa Zimpeto mjini Maputo katika mchezo wa marudiano, hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza fainali hizo ambazo awali ilikuwa zipigwe Morocco.
Televisheni namba moja Tanzania ya michezo na burudani- Azam TV itaonyesha moja kwa moja mechi hiyo kutoka Tunisia kuanzia Saa 1:00 usiku kwa Saa za Kaskazini mwa Afrika na Saa 3:00 usiku kwa Saa za Afrika Mashariki.
Etoile du Sahel wamethibitisha kufikia makubaliano na Azam TV kurusha mchezo huo ‘Live’ leo.
0 comments:
Post a Comment